MWENYEKITI
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa chipukizi zaidi ya 320
litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia
saa 4 asubuhi.
Mwenyekiti
wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida ambaye pia ni Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi mbalimbali
vya sanaa kikiwepo kikundi cha Kaole, Splendid, Super Shine Taarab
pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na
Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.
Taalib
alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas,
Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid
wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio
cha Msanii .
Vikundi
vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni Shaibu, Tanzania
Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew,
Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto
Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale
Morden Taarab na Begeja Wushu,
Taalib
alisema tamasha hilo ambalo limepata kibali cha Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa za Maonesho
Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki
Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.
Mwenyekiti
aliwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab, vikundi vya
sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika tamasha hilo
ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Post a Comment