Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati alipofika kwa mazungumzo leo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
--
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Mkuu wa jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Said Mwema ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Mei 27, 2013.

 Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametumia nafasi hiyo kumpa pole Mkuu wa Polisi kufuatia ajali ya gari la iliyosababisha vifo vya askari wanne wa Jeshi hilo, waliokuwa njiani kutoka Nachingwea kuelekea Mkoani Mtwara kwa kazi maalum ya kudhibiti vurugu zilizojitokeza Mkoani humo juma lililopita.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema, askari hao watazidi kukumbukwa kwa kuwa walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha majukumu yao kwa Taifa hili yanafanikiwa. Mheshimiwa Makamu wa Rais alisema pia kuwa, serikali inathamini sana mchango wa Jeshi la Polisi sambamba na majeshi mengine kutokana na kufanya kazi kwa kujitolea na kwa kutambua kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Mkuu wa Polisi kuwa, kazi inayofanywa na jeshi lake ni kubwa na kwamba Watanzania wanaithamini sana. Pia aliongeza kuwa katika nchi zote wananchi wanaojitolea kufanya kazi katika vyombo vya usalama, ni miongoni mwa wazalendo wakubwa wanaopaswa kuenziwa kwa kuwa wamekubali kuweka maisha yao kwa ajili ya nchi na watu wake.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kupata taarifa kuhusu hali ya usalama mkoani Mtwara na pia kubadilishana mawazo kuhusu kuhakikisha maeneo ya nchi yetu kubakia salama wakati wote. 

Imetolewa na 
Boniphace Makene
           Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top