Mama
Tunu Pinda akiwa anaonyweshwa na Paroko Peddy Castellino mahali Bomu
lilipo angukia na kusababisha maafa na majeruhi katika kanisa Katoliki
Parokia ya Olasiti mkoani Arusha katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba Angela Kairuki kulia kwa Mama Pinda ni Mkuu wa Wilaya Arusha Jonh
Mongela picha na Chris Mfinanga
Mama
Tunu Pinda akiwa na viongozi wa parokia ya Olasiti wakiwaombea Marehemu
walio fariki kutokana na Bomu lililo tupwa katika kanisa Katoliki
parokkia ya Olasiti Mkoani Arusha marehemu hao wamezikwa katika eneo la
Kanisa mahali Bomu lilipo tupiwa Picha na Chris Mfinanga
Mama
Tunu Pinda akiwa anampa pole Bibi Consesa Mbaga (43) ambaye nimiongoni
wa majeruhi walio lazwa katika Hospitali ya Maunt Meru kutkana na
majeraha ya bomu iliotokea katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Olastiti
na kusababisha vifo na majeruhi picha na Chris Mfinanga
Picha ya maktaba ikionyesha wahanga wa bomu hilo wakihangaika mara baada ya mlipuko.
……………………………………………..
MKE
WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amesema Watanzania wote kwa pamoja wana
kila sababu ya kujinyenyekeza mbele za Mungu na kuendelea kuomba ili
pasitokee tena ulipuaji wa mabomu kama lile la Arusha.
Ametoa
wito huo jana jioni (Alhamisi, Mei 16, 2013) alipokuwa akiongea na
Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, Padre Prosper Lyimo wakati
alipokwenda kwenye nyumba ya Askofu ili kuwapa pole kwa maafa
yaliyowapata waumini wa Parokia teule ya Olasiti jijini Arusha, Mei 5 mwaka huu.
Padre
Lyimo alimpokea Mama Pinda kwa niaba ya Askofu Mkuu wa jimbo hilo,
Mhashamu Josephat Lebulu ambaye alikuwa safarini kikazi akitoa huduma
kwa waumini wengine.
Mama
Pinda alisema alilazimika kufika kuwapa pole kwa vile alikuwa amewasili
mkoani Arusha kwa shughuli ya kikazi. “Wote tumepokea kwa mshtuko
taarifa za ulipuliwaji wa bomu pale Olasiti kwa sababu Watanzania
hatujazoea mambo ya mabomu. Tunapaswa wote kwa umoja wetu tumuombe Mungu
ili atuepushie mabaa mengine…” alisema.
Padre
Lyimo aliahidi kuzifikisha salamu za Mhe. Mama Pinda kwa Mhashamu
Askofu Mkuu Lebulu na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali hadi
chanzo kamili cha tukio hilo kibainike.
Aliwasihi
Watanzania kuendelea kuwa na moyo wa kupendana na kushirikiana kwa
sababu wote ni wapitaji. “Sote tuko duniani, sote ni wapitaji. Tupendane
na tuombeane,” alisema.
Baadaye Mama Pinda alizuru Kanisa
la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia teule ya Olasiti na kupata maelezo
kamili kuhusu tukio hilo. Pia alitoa heshima kwa marehemu watatu
waliozikwa kwenye uwanja wa kanisa hilo.
Akitoa
maelezo hayo mbele ya Mama Pinda, Paroko wa Kanisa hilo, Padre Peddy
Castellino alisema ujenzi wa kanisa hilo ulichukua zaidi ya miaka sita
kwa kutumia michango ya waumini wenyewe na wala hawakuwahi kupata msaada
wowote kutoka nje.
Alisema
wao kama kanisa wataendelea kuomba ili tukio hilo liwe la kwanza na la
mwisho. “Tunazidi kuomba ili tukio hili lisijirudie tena hapa nchini, na
pia tunaendelea kumuomba Mungu ili waliohusika na uovu huu waweze
kukamatwa, tunataka kuona mizizi ya matukio haya iking’olewa kabisa na
matukio kama haya yasijirudie tena,” alisema.
Alimshukuru
Mhe. Mama Tunu Pinda kwa kuwatembelea na kuwafariji na kuongeza kwamba:
“Tutaendelea kutetea amani katika nchi yetu ili tunu yetu ya amani
isipotee.”
Wakati huohuo, Mama
Pinda leo asubuhi amewatembelea majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya
Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, jijini Arusha na kuelezwa kwamba kwenye
hospitali hiyo wamebakia wagonjwa 18 na wengine wawili wako katika
hospitali ya Elizabeth wakiendelea na matibabu. Wagonjwa wanane
walihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu Mei 8, mwaka huu.
Mganga Mkuu wa hospitali ya Mount Meru, Dk. Josiah Mlay alimweleza Mama Pinda kwamba wagonjwa wote hali zao zinaendelea vizuri.
Watu 66 waliathirika kutokana na mlipuko huo uliotokea Mei 5, mwaka huu ambapo watatu wamefariki dunia.
Post a Comment