Mama Shida Salum.
********
SHIDA Salum ambaye ni mama
mzazi wa mwanasiasa machachari ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema),
Zitto Kabwe amesema kuna watu wanataka kumuua.
Akizungumza na gazeti hili
kwa njia ya simu Jumamosi iliyopita, Shida alisema Aprili 19, mwaka huu, saa
moja na nusu katika Ghorofa la NSSF maeneo ya Tabata Bima, hawezi kuisahau kwa
kuwa ndiyo siku ambayo majambazi walimvamia wakiwa na
bastola.
Akisimulia mkasa huo Shida
alikuwa na haya ya kusema:
“Majambazi hayo
yaliyonivamia siyajui lakini mmoja wao huwa namuona. Kabla hawajaja walinipigia
simu wakaniambia wana shida na mimi lakini hatukupanga namna ya
kuonana.
Uwazi: Sasa walipofika nyumbani kwako,
uliwakaribishaje?
Shida: Walipofika walivamia na kufanikiwa
kuingia sebuleni.
Uwazi: Baada ya kuingia ikawaje?
Shida: Cha kwanza walichotaka ni laptop
(Kompyuta mpakato), flash na simu zangu.
Uwazi: Uliwapa?
Shida: Baada ya kutoa amri hiyo niliwajibu kuwa
kompyuta iko ofisini na simu niliwaambia ziko kwenye chaji.
Uwazi: Baada ya hapo ikawaje?
Shida: Mmoja wa majambazi hayo alinionyesha
bastola kuwa kama sijatii hayo wanayoniambia basi watanifanya kitu kibaya,
ndipo nikamuita kijana wangu aitwaye Mtana aende chumbani kuchukua simu zangu
niwape.
Uwazi: Ikawaje?
Shida: Niligundua kuwa Mtana alikuwa anasikia
amri zilizokuwa zikitolewa na majambazi hayo, hivyo alipiga kelele kuomba msaada
kwa wananchi.
Uwazi: Majambazi wakafanya nini?
Shida: Waliposikia kelele walikimbilia nje,
wakaingia ndani ya gari lao ambalo namba zake zisijui, wakatoweka.
Uwazi: Pole sana.
Shida: Pamoja na purukushani hizo namshukuru
Mungu sana kwa kuwa hawakunidhuru na hawakufanikiwa kuchukua chochote.
Uwazi lilitinga nyumbani kwa mama huyo na kukuta
ulinzi ukiwa umeimarishwa ambapo sasa kuna askari wenye bunduki.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, majambazi hayo
yalifanikiwa kuingia ndani baada ya mlinzi aliyekuwepo zamu kwenda kubadili nguo
za kiraia ili avae za kiaskari.
“Tukio lilikuwa la haraka sana, wakati askari
huyo anatoka kwenye kibanda cha kubadilishia nguo ndipo na wale majambazi
walipokuwa wakitoka ndani na kuingia kwenye gari lao,” kilisema chanzo.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi wa walinzi
wanaolinda nyumbani kwa mama huyo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Ngosha na
alipoulizwa kuhusu sakata la kuvamiwa alikiri kulifahamu.
“Baada ya tukio lile tumeimarisha ulinzi ili
kuhakikisha usalama wa watu na mali zao. Sasa tumeweka askari wenye bunduki na
tunaamini tukio kama hilo halitajirudia,” alisema Ngosha.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minagi alikiri kutokea kwa tukio
hilo.
“Nina taarifa ya tukio hilo
na tunaendelea na upelelezi kuwasaka majambazi hao, wananchi waondoe hofu.”
alisema Kamanda Minagi.
na global publisher
na global publisher
Post a Comment