Pichani kati ni Miss Earth
Tanzania 2012,Bahati Chando akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo
pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar kuhusiana
na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama Duniani
itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu ya
Mwaka huu imepangwa kuwa ni "always in our heart's", "tukiwakumbusha
akina mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda sana" alisema
Chando.Shoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa na kulia ni
Mratibu wa hafla hiyo,Bi.Regina Ogwalla.Bahati amesema kuwa katika hafla
hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala,Mh.Nora
Mzeru.
Miss Earth Tanzania 2012,Bahati
Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa kata ya
Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na Wamama wa
Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia
kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku
kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama
watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa mrembo wa
kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa.
Pia anasema kuwa ameandaa sherehe
hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss sio tu kupozi mbele ya
Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa jamii kwa namna
mbalimbali.
Shoto
ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa akitoa ufafanuzi
kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day",siku ya Mama
Duniani itakayofanyika Mei 12,2013 kwenye hoteli hiyo,ambapo kauli mbiu
ya Mwaka huu kwenye hafla hiyo umepangwa kuwa ni "always in our
heart's".
Post a Comment