............................................. Geita yaguswa na kampeni ya fistula
Mkuu wa Mkoa ajitolea kuwa Balozi, aahidi ushirikiano Kampeni inayoendelea katika mikoani ya kuelimisha wananchi juu ya fistula imewahamasasisha wakazi wa mji wa Geita huku Mkuu wa Mkoa huo Said Magarula akionesha dhahiri kuguswa na kutangaza kuwa yupo tayari kuwa balozi wa fistula katika mkoa wake ili kumaliza tatizo hilo.
Msafara wa kampeni ya fistula unaojumuisha wataalamu kutoka Hospitali ya CCBRT, mabalozi wa fistula ambao ni wanawake waliowahi kupatwa na tatizo hilo pamoja na Balozi wa Chapa ya Vodacom Msanii Mwana FA uliingia mjini Geita jana na kuendesha kampeni ya wazi kwa wananchi.
Msafara huo unafadhiliwa na kampuni ya Vodacom na Vodafone ya Uingereza ikiwa ni sehemu ya kuelekea kielle cha siku ya fistula dunaini Mei 23, kitakachofanyika jijini Dar es salaam.
Wakionesha kuguswa na ushuhuda uliotolewa na mabalozi wa fistula pamoja na elimu ya jumla kuhusu tatizo la fistula kwa wanawake, wakazi hao wamesema wapo tayari kuungana na wafadhaili wa kampeni ya kutokomeza fistula nchini ifikapo mwaka 2016.
"Fistula muisikie tu kwa mbali na wala msiombe kuishuhudia kwa macho, ni mbaya na inatutesa sana wanawake kampeni hii inatupa faraja na kutufanya tujisikie kuwa sasa tupo salama wakati wa kujifungua."Alisema Salma Daudi wakati akitoa maoni yake wakati wa kamepni hiyo.
Aidha baadhi ya vijana na wanaume waliofika kwenye tukio hilo wamesema baada ya kupata ushuhuda kutoka kwa wanawake waliowahi kupatwa na tatizo la fistula pamoja na elimu iliyotolewa ikiwemo ujumbe kwamba fistula inatibika tena bila malipo kwa gharama za Vodacom na Vodafone, wamehamasika.
"Ki ukweli nimeguswa sana na kama mwanaume nimehamasika kutoa mchango wangu katika jamii na hata kuwa tayari kumvumulia mke wangu iwapo atapatwa na tatizo hilo wakati wa kujifungua kwa kuwa fistula inatibika, mmetugusa sana na tunashukuru kwa kutufikia."Alisema Magige John mkazi wa Geita
Magige aliiomba Vodacom kuhakikisha inafanya kila jitihada kuhakikisha kampeni hiyo inafika Tanzania nzima ili kuhakikisha kila mtu anapata elimu ya fistula na hasa kufahamu kwamba inatibika tena buila malipo huku akitoa rai kwa wanaume kuwa na mtazamo tofauti sasa juu ya fistula.
Akizungumza katika kampeni hiyo Mkuu wa Mkoa Bw. Magarula aliahidi kutumia nguvu na rasilimali za mkoa ukiwemo mtandao wa kiserikali kutoka ngazi ya mkoa hadi kitongoji kuhakikisha ujumbe wa fistula unamfikia kila mkazi wa Geita.
Amesema sio uamuzi rahisi kwa kampuni ya biashara kuamua kwa makusudi kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuwezesha matiababu kwa wanawake wenya na wanaopatwa na tatizo la fistula hivyo fursa hiyo lazima ipewe heshima na kutumika kwa masilahi ya taifa.
"Mfumo wa serikali unaanza na mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, watendaji tarafa, kata kijiji hadi kitongoji hivyo nitautumia mfumo huu kuhakikisha kila mkazi wa Geita anafikiwa na ujumbe wa fistula inatibika na matibabu yake ni bila malipo kwenye hospitali ya CCBRT"Alisema Magarula
"Natambua kuwa changamoto kubwa tuliyanayo katika huduma za afya ni gharama za matiabbu, wenzetu hawa Vodacom wameshajitolea sasa tena kwa asilimia mia moja, hivyo sioni kwa nini tuendelee kujificha, kuogopa na kuteseka."Alisema Magarula huku akitangaza kuwa atakuwa balozi wa fistula mkoani mwake.
"Naipongeza Vodacom na Vodafone ya Uingereza kwa kuamua kwa makusudi kuendesha kampeni na pia kufadhili kampeni hii kwa wananchi wetu, hili ni jambo kubwa na muhimu linalopaswa kuungwa mkono, serikali haina kikwazo kutoa ushirikiano kwa jambo lolote lenye masilahi ya taifa. Natanga ushirikiano wa seriklai ya mkoa na mimi kuanzia sasa ni balozi wa kujitolea wa fistula hapa mkoani."Aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa
Kwa wastani Vodacom na Vodafone hutumia kiasi cha Sh. 700,000 hadi sh 900,000 kugharamia matibu ya mgonjwa mmoja wa fistula.
Akitoa salaam zake, Balozi wa Chapa Vodacom Mwana FA alisema itashangaza sana kama Tanzania itaendelea kuwa na mwanamke mwenye tatizo la fistula licha ya juhudi kubwa zinazofanywa katika kumaliza tatizo hili.
"Binafsi kwa mara ya kwanza niliposimuliwa na kupatiwa ushuhuda wa fistula moyo wangu ulishtuka sana, mama zetu wanateseka lakini ninafaraja kuona kwamba zipo juhudi za makusdi kutoka Vodacom kuhakikisha kila mwanamke mweneye fistula anasaidiwa kwa kupata matibabu bila ya malipo kupitia hospitali ya CCBRT."Alisema Mwana FA
Hata hivyo Balozi huyo amesema shabaha njema ya Vodacom inaweza isizae matunda iwapo jamii yenyewe hasa wanaume wasipoonesha utayari wa kuinga mkono kwa kuwa karibu na wake zao pindi wanapopatwa na fistula na kuwatoa ili kupata matibabu.
Vodacom na Vodafone imeweka shabaha ya kuhakikisha Tanzania haina mwanamke aliye na tatizo la fistula ifikapo mwaka 2016. Kwa sasa makampuni hayo yanafadhili gharama za matibabu katika hospiatali ya CCBRT ya jijini Dra es salaa ikiwemo gharama za chakukla, malazi na nauli ya kumwezesha mgonjwa kutoka alipo hadi Hospitali na kumrudisha.
Post a Comment