Wawakilishi
wa Mradi wa TSCP na Wawakilishi wa World Bank katika picha ya pamoja,
hivi karibuni walipotembelea Mwanza katika kubaini utekelezaji na
maendeleo ya maeneo mbalimbali ya mradi huo.JPG
Timu
ya wataalamu kutoka OWM-TAMISEMI-katika Mradi wa Mpango Miji Mkakati
(TSCP ) Pamoja na wawakilishi kutoka Benki ya Dunia pamoja na Ubalozi wa
Denmak wakikagua Ujenzi wa Barabara zinazoendelea kujengwa kupitia
mradi wa TSCP katka Mnispaa ya Mtwara Mikindani katika kubaini utekelezaji na maendeleo ya maeneo mbalimbali ya mradi
Hii ni baadhi ya mifereji iliyokamilika baada ya ujenzi huko Tanga.
………………………………………………………….
Toka uzinduzi wa mradi wa uendelezaji Miji. Tanzania Strategic Cities Project (TSCP),uanze
mnamo mwaka 2010. Umekuwa ukiboresha huduma za msingi mijini kufikia
walengwa. Mradi huu wa uendelezaji miji Tanzania umeundwa kwa ajili ya kukabili
changamoto mbalimbali za Miji ya Tanzania. Mradi huu unatekelezwa na Halmashauri
nchini, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tamisemi.
Mradi huu ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na ruzuku kutoka Danida.
Mwanzoni mwa wiki mwandishi wetu aliongea na Kaimu Katibu Mkuu wa Tamisemi Bwn.
Jumanne Sagini ambaye alikua na haya ya kusema “Mradi wa uendelezaji miji Tanzania
upo na una lengo la kuboresha viwango na kurahisisha ufikiwaji wa huduma za msingi
Mijini kwa kukarabati na kupanua miundombinu ya Miji pamoja na kuziimarishia uwezo
taasisi husika katika kuboresha mapato na usimamizi wake”
Bwn. Jumanne Sagini aliendelea kusema “Mradi huu umegawanyika katika maeneo
makuu matatu ambayo ni Miundo mbinu na huduma za miji; Uimarishaji wa Taasisi
pamoja na Usimamizi wa Mradi; na ni miji saba tu ndiyo itakayofaidika na mradi huu.
Miji yenyewe ni Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya, Mtwara, na Dodoma, Kwa
Mji wa Dodoma, Mradi unatekelezwa na Halmashauri ya Manispaa Dodoma Ustawishaji
Makao Makuu Dodoma (CDA)”.
Mradi huu unagharama ya $ 175.5, ambapo $162.8 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na
$12.7 ni ruzuku kutoka DANIDA. Mkopo wa Benki ya Dunia ni kwa ajili ya maeneo ya
Miundombinu na huduma za miji, wakati ruzuku kutoka DANIDA itagharamia uimarishaji
wa Taasisi katika kutekeleza majukumu yake.
Ili kujua kwa undani zaidi kuhusu mradi huu, Mwandishi wetu wa habari aliongea na
Mratibu wa mradi huu Mhandisi Davis Ben Shemangale.
Mhandisi Davis Ben Shemangale alielezea : “Mradi huu ni njia ya kutekeleza dhana ya
kugatua madaraka toka Serikali Kuu kwenda kwa umma, mradi huu wa TSCP
unaendeshwa na Halmashauri husika kwa kuchagua na kuitekeleza miradi kwa kadri ya
vipaumbele vyao”.
Mhandisi Davis Ben Shemangale alimalizia kwa kusema “mradi huu umewekwa katika
awamu tatu hadi nne kwa kila mji na mpaka sasa wakandarasi kwa awamu zote
wamekwisha anza kazi” aliendelea kwa kusema “wakandarasi kwaajili ya kutekeleza
awamu ya kwanza walianza kazi Novemba mwaka 2011 na awamu ya pili walianza kazi
mwezi June mwaka 2012 ambapo awamu ya tatu na ya nne walianza kazi mwezi
Novemba 2012”

Post a Comment