
Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa
Habari Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia
njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge
Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’
Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na
kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao
na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki
iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa
mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee
amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata
kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto
watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko
radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari
ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la
malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa msanii huyo
akiitwa katika vyombo vya sheria.
Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza
kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la
mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua
kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama
facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo
ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo
Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady
Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner
Habash simu iliita bila kupokelewa.


Post a Comment