Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tamisemi yapatiwa vifaa vya michezo vya Sh70m kutoka Liike sports

tamis ea18f
Naibu waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa
***********
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa amepokea vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 70 kutoka shirika lisilo la kiserikali liitwalo Liike Sports and Development kutoka nchini Finland.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ndogo ya TAMISEMI zilizopo jijini Dar es Salaam yaliyoshuhudiwa na maafisa elimu kutoka mikoa ya Morogoro, Lindi,Dar es Salaam na Pwani pamoja na maafisa michezo kutoka mikoa hiyo .
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo,Naibu Waziri Majaliwa alisema kuwa atahakikisha vifaa hivyo vinatumika kama inavyotakiwa katika kukuza na kuendeleza michezo shuleni na kuongeza waalimu wa michezo na mitaala ya somo la michezo ili kuwaanda wanamichezo bora.

Naibu Waziri alitoa wito kwa Maafisa Elimu na viongozi wa shule kwa kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kutoa kipaumbele cha kuwapanga walimu wa michezo kwenye shule zilizoteuliwa kufundisha michezo.
Aidha Naibu waziri amezitaka halmashauri nchini kutenga fedha katika mipango ya bajeti kwa ajili ya mafunzo kwa walimu wa michezo sanjari na kufundisha masomo mengine na kuahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa karibu kwa shirika la Liike ili kuimarisha michezo nchini.
Alisema kuwa serikali imeamua kurejesha michezo shuleni kupitia mashindano ya michezo kwa shule za msingi na sekondari (UMITASHUMTA na UMISETA) ili kuwapa watoto mafunzo kuanzia ngazi ya msingi na hatimaye kupata wachezaji bora watakaojiajiri katika michezo.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni mipira 2620 ya kuchezea mpira wa miguu, mikono, wavu, kikapu na pete, tufe 120, mikuki 120, visahani 120,filimbi 300, saa za michezo 300, nyavu za mpira wa wavu 60,raketi za mpira wa wavu 360, nyavu za vinyoya 60,vitabu vya Kiongozi cha Mwalimu120 na vitabu vya kufundishia 120.
Naibu Waziri Majaliwa alisema vifaa hivyo vitatolewa kwa shule mbili za msingi na mbili za sekondari katika kila mkoa kwa ajili ya kufundisha michezo, kuendeleza na kutoa elimu ya michezo katika vyuo vya ualimu ili kuhakikisha kila shule ya msingi na sekondari inakuwa na mwalimu aliyesomea michezo.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Liike, Ari Koivu, alisema shirika hili linataka kusaidia watoto shuleni kujenga afya na akili kupitia michezo kwa kutoa vifaa mbalimbali vya michezo hususani kwa shule za serikali kwa ili kupunguza tatizo la uhaba wa vifaa vya michezo.
Liike ni shirika linaloisaidia Tanzania katika kukuza na kuendeleza michezo na elimu ya viungo katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu ambapo litatoa somo la michezo kwa shule 58 za sekondari katika mikoa yote ya Tanzania. Chanzo:Lorietha Lawrence
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top