Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu
Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Wakili wa Msigwa kulia akiteta jambo nje ya mahakama
Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe
akiingia na viongozi wengine wa chadema mahakamani hapo huku wafuasi
wao wakizuiwa nje ya mahakama
Wafuasi wa Chadema wakiwa
wamezuiliwa nje ya viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa wakati
mbunge alipofikishwa katika mahakamani mchana huu
Ulinzi mkali kweli kweli
ulinzi mkali wakati mbunge Msigwa na watuhumiwa wengine 70 wakifikishwa mahakamani leo
Wafuasi wa Chadema na wananchi wakiwa nje ya geti la mahakama leo
Watuhumiwa 70 wa vurugu za machinga na polisi mjini Iringa akiwemo mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa hivi sasa wanafanyiwa utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana baada ya kusomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana unafanyika mbele ya mahakama hiyo ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya .
Hata hivyo wamekana mashitaka yote yaliyotolewa ambayo shitaka la kwanza la mbunge ni kushawishi kufanya vurugu ,huku wengine wote kosa la kwanza kufanya mkutano bila kibali , kuharibu mali kinyume na sheria ni kufanya vurugu .
Hadi sasa baadhi ya watuhumiwa wana wadhamini na dhamana yao ni kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 1 na kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.
Habari kamili inakujia hivi punde ila hadi sasa mdhamini wa mbunge Msigwa na baadhi ya watuhumiwa waliowengi wametimiza masharti ya dhamana
CREDITS: MATUKIO DAIMA BLOG
Post a Comment