Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi (chadema) akitolewa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Iringa leo na watuhumiwa wengine watatu kupelekwa mahakamani akihusishwa na vurugu za machinga na polisi jumapili iliyopita
Katibu mwenezi wa Chadema Iringa mjini Joseph Mgimwa (kushoto) akiwa na mtuhumiwa wenzake wa vurugu za machinga na polisi jumapili iliyopita Bw . Frank Nyalusi ambae ni diwani wa kata ya Mvinjeni kupitia Chadema na watuhumiwa wengine wawili wakifikishwa mahakamani leo Iringa na kufikisha idadi ya watu 78 ambao wamepandishwa kizimbani kwa vurugu hizo akiwemo mbunge Peter Msigwa
Polisi wakiwalinda watuhumiwa wa vurugu za machinga na polisi Iringa , watuhumiwa hao ni Joseph Mgimwa katibu mwenezi (chadema) Iringa mwenye suti nyeusi anayefuata aliyevalia sare za Chadema ni diwani wa kata ya Mvinjeni Bw Frank Nyalusi na watuhumiwa wengine William Mbunda na Timotheo Msengwa
katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima na ndugu wa watuhumiwa wa vurugu ambao wameachiwa leo kwa dhamana wakitoka mahakamani hapo huku wakifurahi baada ya kukamilisha dhamana
Diwani Nyalusi akitoka mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana leo
Viongozi wa Chadema Iringa kutoka
kushoto diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi na katibu mwenezi wa
Chadema Iringa Joseph Mgimwa akiwasalimia wafuasi wa Chadema
waliofika mahakamani hapo leo
Diwani Nyalusi wa pili kushoto akitoka mahakamani Iringa baada ya kuachiwa kwa dhamana leo
SAKATA
la vurugu za machinga na polisi Iringa limeendelea kuchukua sura
mpya zaidi baada ya jeshi la polisi mkoani Iringa kuwakamata na
kuwafikisha mahakamani makada wengine wanne wa chama cha Demokrasia
na maendeleo (chadema) akiwemo diwani kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi
(Chadema) na katibu mwenezi wa Chadema Iringa mjini Joseph Mgimwa .
Watuhumiwa hao wanne wamefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Wilaya ya Iringa mheshimiwa Festo Lwila kusomewa mashtaka matatu likiwamo la uchochezi na kuharibu gari la Zima moto mjini Iringa
Watuhumiwa hao ambao ni Katibu mwenezi wa Chadema Joseph Mgimwa na Diwani wa kata ya Mivinjeni Chadema Frenk
Nyalusi ni miongoni mwa watuhumiwa hoa mbao kufikishwa kwao mahakamani
kunafanya idadi ya watu waliofunguliwa mashitaka kutokana na tukio la
vurugu zilizotokea Jumapili ya mei 19 mwaka huu kufikia 80.
Katika
shtaka la Msingi watuhumiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni Frenki
Nyalusi ambaye ni diwani wa Kata ya Mivinjeni (Chadema)na Joseph Mgimwa Katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Iringa ambaye pia ni katibu wa Mbunge wa Jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa walisomewa mashitaka mawili likiwamo la uchochezi huku watuhumiw awengine wakisomew amashitak yote matatu.
Akisoma
shitaka hilo mbeleya Hakimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa Festo
Lwila,mwendesha mashitaka wa serikiali Elizabeth Swai alisema mnamo Mei
19 mwaka huu katika eneo la Mashine tatu Manispaa ya Iringa watuhumiwa watuhumiwa hao ambao ni namba 2 na namba 4 walitenda kosa la ushawishi watu kutenda kosa kinyume na sheria za nchi.
Alisema
katika kosa la pili watuhumiwa hao walifanya mkutano na maandamano bila
kibali cha polisi mkoa kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi na
katika koisa la tatu watuhumiw ahao kw amakusudi waliharibu mali ambayo
ni gari la zimamoto la Manispaa ya Iringa kitendo ambacho ni kosa
kisheria.
Mwendesha
mashitaka huyo wa serikali pia aliwataja watuhumiw awengine katika kesi
hiyo ambayo mtuhumiwa namba mmoja ni Mbunge wa Jimbo hilo Mchungaji
Peter Msigwa kuwa ni William Mbunda na Timotheo Msengwa ambao walihushwa na makosa yote matatu.
Hakimu
Kiongozi wa Mahakama hiyo Lwila aliwaachia watuhumiwa hao kw adhamana
kama ilivyoelekezwa na mahakama Mei 20 mwaka huu ambapo masharti ya
dhamani ni kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho na
ahadi ya Sh 1 milioni pamoja na kutakiwa kutotenda kosa lolote katika
kipindi chocte cha dhamana,Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 3 itakaposomwa tena mahakamani hapo
Wakati
huo huo viongozi hao wa Chadema wilaya ya Iringa mjini chini ya
katibu wake Suzana Mgonakulima wamefanikiwa kuwawekea dhamana
watuhumiwa 26 ambao walikamatwa na mbunge Migwa na kushindwa
kutoka kwa dhamana siku ya jumatatu baada ya kukosa kutimiza vigezo
vya mahakama.
katika hatua nyingine serikali
mkoa wa Iringa imeapa kupambana na makundi ya watu wavuruga amani
kwa kuhamasisha vurugu zinazopelekea damu kumwagika .
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alitoa onyo hilo jana wakati
akizungumza na wanahabari ofisini kwa juu ya kuwepo kwa taarifa kama
hivyo za watu kuhamasisha vurugu .
Hivyo
alisema mkoa wa Iringa umejipanga kuwabana wale wote watakaokutwa
wakichochea vurugu na kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Mkuu
huyo wa mkoa alitaka wakazi wa mkoa wa Iringa kutoa taarifa mapema
polisi iwapo watabahatika kuwaona ama kusikia mipango yoyote ya
kuvuruga amani ikipangwa na watu hao ama kupokea ujumbe mfupi katika
simu zao ambao unachochea vurugu.
Kuhusu
vurugu zilizojitokeza jumapili eneo la Mashine tatu mkuu huyo wa
mkoa alisema kuwa serikali kupitia jeshi la polisi na vyombo vingine
vya ulinzi na usalama wamejipanga kuimarisha amani siku ya kesho
katika mji wa Iringa na iwapo kuna mtu atajaribu kufanya vurugu basi
atawajibishwa .
CREDITS: HABARI MATUKIO BLOG
Post a Comment