MHE. GERSON LWENGE |
NA IMMACULATE MAKILIKA-MAELEZO
SERIKALI imesema inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari
katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336
katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo
hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la
Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
Hayo yalisemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge,
wakati akijibu swali Mbunge wa Jimbo la Temeke Abasi Zuberi
Mtemvu lililouliza kuwa Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya
ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
Alisema kuwa inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya
kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni kama
ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni
–Morocco (Sh. bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa
haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
Nyingine ni Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh. bilioni 88.00),Barabara ya
Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh. bilioni
35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya
Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani
(Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa
ajili ya ujenzi.
Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
Waziri huyo alisema ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka
Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano
wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano
na kujenga barabara ya juu (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga
daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala
(salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive kuunganisha na Ocean
Road.
Post a Comment