Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHIRIKISHO LA WAKURUGENZI WA MASHTAKA AFRIKA MASHARIKI LAPANIA KUBORESHA UMOJA WAO.

 


1cc
Na Genofeva Matemu – MAELEZO,
Shirikisho la wakurugenzi wa mashtaka Afrika Mashariki limeazimia kuongeza wigo wa ushiriki wa kikosi kazi ndani ya shirikisho hilo ili kuwajibika zaidi na kuweza kupata njia nyingine ya kupanua ushiriki wa waendesha mashtaka binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, rais wa shirikisho hilo Martin Ngoga amesema kuongezeka kwa wigo kutasaidia kuleta ushirikiano wa kutosha na hatimaye kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
“ kwa kipindi hiki uhalifu umekua na changamoto kubwa sana hivyo kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia kupanua wigo wa kupata mafunzo ya pamoja kwa wanachama wa shirikisho na kupunguza baadhi ya changamoto hizo”, amesema Ngoga.
Naye makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi amewataka waandishi wa habari kutokujadili na kushadadia kesi zilizoko mahakamani kwani kesi ikiwa mahakamani hairuhusiwi kujadiliwa bali kuiachia mahakama kufanya kazi yake.
Mkutano wa Shirikisho hilo ulioanza jana umemalizika leo ukiwa umehudhuriwa na  wakurugenzi wa Mashtaka kutoka  nchi tano za Afrika mashariki uliokuwa na lengo la kupitia upya Katiba yao ili kuimarisha umoja wao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top