Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mulongo katika Uwanja wa Ndege wa KIA.
Askofu
Mkuu wa jimbo kuu la Arusha Baba Askofu Josephat Lebulu akizungumza
jambo na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda juu tukio lililotokea hivi
karibuni.
Paroko
Pedy Kasterino wa paroko ya Tokeo la Bwana Bulka Olasite akimpa maelezo
Mhe. spika jinsi mlipuko ulivyotokea katika kanisa la Mt. Joseph Olasite
Mjini Arusha.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwafariji katika majeruhi katika Hospitali
ya Mount Meru kufuatia Mlipuko uliotokea katika Kanisa la Mt. Joseph
Olasite, Mjini Arusha na kusababisha Vifo vya watu 3 kufariki na wengine
zaidi ya 60 kujeruhiwa jumapili iliyopita.
Paroko Pedy Kasterino wa paroko ya Tokeo la Bwana Bulka Olasite akimuongoza Mhe. Spika kuangalia eneo mlipuko huo ulipotokea.
Spika
wa Bunge akiwapa pole wananchi waliofika eneo la parokia ya Mt. Joseph
Olasite alipofanya ziara ya kutembelea eneo ambalo mlipuko ulitokea
jumapili.
Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Mjini, Mhe. John Mongela akimkaribisha Mhe. Spika
pamoja na ujumbe wa Wabunge alioambatana nao katika Uwanja wa KIA.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mulonga akitoa taarifa kwa Mhe. Spika pamoja
na Wabunge jinsi tukio la mlipuko ulivyotokea katika parokia ya Mt.
Joseph Olasite Mjini Arusha Jumapili iliyopita.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora,
Mhe. Capt. George Mkuchika , Mhe. Pindi Chana na Mhe. Richard Ndasa
wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Mkoa.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiushukuru Mkoa wa Arusha kwa juhudi
zilizofanya mpaka sasa katika kuwasaka wahalifu waliotekeleza shambulio
hilo.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimpa pole Askofu Mkuu wa jimbo kuu la
Arusha Baba Askofu Josephat Lebulu kutokana na Mlipuko uliotokea
jumapili iliyopita katika Parokia ya Mt. Joseph Olasite.
Baba askofu akisalimiana na waheshimiwa wabunge.
Spika wa Bunge pamoja na wabunge wakimfariji baba askofu pamoja na uongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasilisha rambirambi zilizotolewa na
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Askofu wa jimbo kuu la
Arusha Baba Askofu Josephat Lebulu kufuatia mlipuko ulisababisha vifo
vya watu 3 jumapili iliyopita na kuacha watu zaidi ya 60 majeruhi.
Picha zote na Owen Mwandumbya
Picha zote na Owen Mwandumbya
Post a Comment