Ijumaa
iliyopita Mei 3, 2013 Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni Masuala ya
katiba na Sheria Ndg. Tundu Lissu katika hotuba yake pamoja na
kuzishutumu taasisi zingine, lakini pia alitoa tuhuma kadhaa dhidi ya
CCM.
Tuhuma
hizo zilielekezwa kwenye maeneo kadhaa hasa yahusuyo suala la mchakato
wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea nchini na ushiriki wa makundi
tofauti katika mchakato huo.
Katika
kuipa uzito hoja hiyo, Lissu alitoa malalamiko mengi dhidi ya CCM kwa
madai kuwa tumeteka mchakato huo kwa kujaza Makada wa CCM katika
Mabaraza ya Katiba yaliyoundwa kwenye ngazi ya kata hivi karibuni.
CCM
Kama ilivyo taasisi yoyote makini na wenye uzalendo kwa nchi yao,
katika mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ina jukumu la kuwahamasisha
wanachama na wasio wanachama wake kushiriki mchakato wa katiba nchini
kutokana na kutambua umuhimu wake.
Tofauti
ya CCM na Chadema katika hili ni, wakati CCM tunahamasisha watu
washiriki kwenye mchakato wa katiba nchini, Chadema wao wanahamasisha
watu wavuruge au wasishiriki kabisa mchakato huu.
Mfano
mzuri ni jitihada zao za kuziria mchakato huu kwa visingizio vya kitoto
kabisa. Juhudi zao za kumtaka Prof. Baregu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema, ambaye wao Chadema walimpendekeza kwenye tume, ajitoe kwenye
tume zinafahamika na wala sio SIRI.
CCM
inampongeza kwa dhati Prof. Baregu kwa uzalendo na ukomavu wa kisiasa
aliouonyesha kwa kuwakatalia kujitoa kwenye tume na kuweka mbele
masilahi ya taifa lake. Kukataa kwa Prof. Baregu kujitoa kwenye tume kwa
hoja za kitoto kabisa za Chadema ilipaswa kuwa fundisho kwa vibaraka
hawa.
Ilivyo
fanya CCM, kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki
mchakato huo, ndivyo taasisi nyingine pia zilivyofanya. Zikiwemo taasisi
za dini ambazo zimekuwa zikihamasisha zoezi hili kupitia mikusanyiko ya
Ibada, Taasisi zisizo za Kiserikali yaani NGOs kwa kufanya makongamano
na makundi mengine kwa kuendesha midahalo, dhambi kwa CCM inatoka wapi?.
Ifahamike
kuwa mawasiliano na mjadala juu ya zoezi la mchakato wa uundwaji wa
katiba mpya nchini hayakuanza jana ndani ya CCM, bali yalianza siku
nyingi kwa Chama kuunda kamati iliyopitia na kuja na maoni ya CCM juu
ya nini kiwemo kwenye katiba mpya.
Taarifa
hiyo haikufanywa Siri. Iliwasilishwa mbele ya vikao kadhaa vya Chama
na kisha kutangazwa kwa umma. Hivyo hoja kwamba mawasiliano ndani ya
Chama juu ya mchakato huo wa Katiba nchini umelenga kuhujumu mchakato
huo hayana maana yoyote, badala yake hoja hiyo imebeba mtazamo finyu wa
wanasiasa wenye tabia za nguruwe za kula watoto wake mwenyewe pindi
apatapo njaa.
Chadema
ni kama nguruwe ambaye huweza kuzaa watoto wake kisha akishikwa njaa
huanza kuwala watoto wake mwenyewe. Mchakato wa katiba nchini ni matunda
ya viongozi wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CCM
Taifa, kutangaza kuanza kwa mchakato huu. Hatuwezi kuuzaa wenyewe
mchakato halafu tukauhujumu wenyewe mchakato huo.
Itakumbukwa
umezuka utamaduni mbaya kwa baadhi ya Wabunge wa CHADEMA kutumia Bunge
kama jukwaa la kuwashambulia isivyo sawa watu ambao hawana fursa ya
kuingia Bungeni kujibu mashambulizi hayo. Utamaduni huu ni wa hovyo
unakiuka haki za msingi ambazo zinataka mtu anayetuhumiwa/kushutumiwa
apewe fursa ya kusikilizwa. Watanzania lazima tuukatae utamaduni huu.
Hivi
karibuni baadhi ya Wabunge wa CHADEMA wamefanya vitendo vya aibu
vilivyowakera sana Watanzania. Hili bado limo kwenye akili na midomo ya
watu na sasa Chadema wanatafuta namna ya kuficha aibu yao(nitoke vipi)
kwa kurukia hoja ya Mabaraza, kuzusha na kushutumu watu kwa uongo
uliokubuhu.
Vituko
vyote hivi vya Chadema vimeongezeka baada ya katibu mkuu wa CCM hivi
karibuni mjini Morogoro kutoa maelezo ya kina na hoja nzito dhidi ya
ukibaraka wa Chadema kwenye suala zima la mchakato wa Katiba.
Nchi
nyingi hasa za Afrika zilizokumbwa na machafuko moja ya ajenda kubwa
ilikuwa ni swala la katiba mpya. Sasa hapa nchini Chadema wanaona
watanzania wanaendelea na mchakato bila machafuko wanakosa majibu kwa
mabeberu wanaowafadhili kuchafua nchi yetu, ndio maana kila kukicha
wanakuja na visa na vituko kusumbua mchakato wa katiba.
Walianza
kwa kukataa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ikiwemo kutomtambua
rais. Wakatangaza hadharani nchi haitatawalika kisa wamenyimwa ridhaa na
watanzania. Mchakato ulipoanza wa katiba mpya wabunge wao wakazira na
kutoka nje ya bunge, baada ya muda wakarudi.
Juzi bungeni wametishia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30/04/2013, leo ni tarehe 05/05/2013!!
Wamezoea kutishia nyau, tumechoka na vitisho vya vibaraka hawa.
Tunapongeza msimamo wa Tume ya mabadiliko ya Katiba kwa kupuuza hoja ya
kufuta mabaraza ya katiba. Chadema wakisusa na wasuse tu.
Tunawasihi
watanzania wote wapuuze utoto na ukibaraka huu wa Chadema kwani ugonjwa
wao tumesha ufahamu WANAUMWA KIFAFA CHA SIASA. Kila ugonjwa huu
ukipanda wanatupa mateke sana. Tuwaombee ipo siku huenda mwenyezi Mungu
atawarehemu watapona.
Mwisho
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary
1 comments:
Nakupongeza sana sana, huku Geita CDM wametuma vibaraka kutoka sehemu mbali mbali wanatembelea vijiwe vyote na kushawishi watu waandamane na wakati wa maandamano wapire mali zawatu kwa madai kuwa mali hixo ni zao walibiwa. Ulipokuja hapa Geita ukalala Alpha hotel walichuka sana. Karibu na utusaidie watu wa Geita juu ya vibaraka hawa.
ReplyPost a Comment