Waombaji
waliotuma maombi ya fursa za ajira kwa ajili ya matangazo yaliyokuwa
yametolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba
ya Waajiri mbalimbali nchini mnamo tarehe 26 Machi, 2013 moja likiwa
katika lugha ya Kiingereza na lingine katika lugha ya Kiswahili ambapo
mwisho wa kutuma maombi ilikuwa tarehe 9 Aprili, 2013 wametakiwa
kutembelea tovuti ya Sekretarieti ya Ajira mara kwa mara ili kupata
ratiba ya usaili kwa nafasi walizoomba.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo alipokuwa akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea ofisini kwake wakitaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira Serikalini.
Amesema ofisi yake itaendelea kuwafahamisha wale wote walioomba nafasi za kazi Serikalini kadri siku zinavyosogea. Amebainisha kuwa kwa tangazo la kiingereza lililotolewa tarehe 26 Machi, 2013 ambalo lilihusu
Taasisi
za Umma zaidi, usaili wake utaanza tarehe 20 mwezi huu kama ratiba
ilivyoainisha katika tangazo la kuwaita kwenye usaili lililotolewa
tahere 16 Mei, 2013 kupitia tovuti ya Sekretarieti ya Ajira likibainisha
usaili utafanyika tarehe ngapi na sehemu gani pamoja na orodha ya
majina ya wahusika waliokidhi vigezo vya tangazo kwa nafasi hizo.
Daudi amewataka waombaji wa tangazo lililokuwa limetolewa kwa
lugha ya Kiswahili tarehe tarehe 26 Machi, 2013 waendelee kuvuta subira
kwani ratiba yake ya Usaili kwa waombaji wenye Sifa itatolewa mara
baada ya Usaili wa Tangazo la Kingereza kukamilika ili kuepuka
kuwachanganya waombaji. Pamoja na hayo amewataka waombaji hao kukaa
tayari kwani usaili wa tangazo hilo unaweza kufanyika wakati wowote
mwezi Juni mwaka huu ila tarehe rasmi na wapi watajulishwa baadae.
Aidha, Waombaji wa nafasi wazi za kazi kwa tangazo la kazi lililotolewa kupitia tovuti hii tarehe 16 Aprili, 2013 ambalo mwisho wake wa kutuma maombi ilikuwa tarehe 2 Mei, 2013, wanafahamishwa kuwa mchakato wa kuchambua maombi yao bado unaendelea na watapewa taarifa ya kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo vya tangazo mara baada ya taratibu zote kukamilika.
Katibu huyo pia ametoa Rai kwa waombaji wote waliochaguliwa kuja kufanya usaili kujiandaa vyema ikiwa ni pamoja na kuzingatia vitu muhimu wanavyopaswa kuja navyo kwenye usaili ikiwemo vyeti vya Kitaaluma.

Daudi alimalizia kwa kuwatahadharisha waombaji wa fursa za Ajira serikalini pamoja na wadau kuwa makini na baadhi ya Matangazo ya Ajira ambayo yanatolewa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii hususani wa www.eastafricajobscareer.
Hivyo amewataka wadau wote kuyapuuza matangazo hayo ya uongo yenye nia ya kuwapotosha. Aidha, amewahimiza wananchi pindi wanapoona matangazo ya kazi yanayoihusisha Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika mitandao au mbao za matangazo kujiridhisha ili kuyathibitisha kupitia tovuti ya www.ajira.go.tz ili kuwa na uhakika zaidi kuliko kudanganywa na kutuma barua za maombi kwa matangazo ambayo si ya kweli.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz au simu 255-687624975
20 Mei, 2013
Post a Comment