30 TWIGA STARS WAITWA KAMBINI
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars),
Rogasian Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa
kuijenga na kuiimarisha timu hiyo.
Twiga
Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu)
ambapo baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya
wachezaji kurudi kwenye klabu zao.
Kambi
hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na
kuiimarisha timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa
kambi ya pili baada ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens),
Aziza Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma
(Sayari), Ester Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo
(Mburahati Queens) na Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).
Fatuma
Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda
(Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna
Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati
Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).
Nabila
Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord
Barden), Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida
Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona
(TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati
Queens).
RCL KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO
Raundi
ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26
mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita
tofauti.
Abajalo
ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro
itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika
mjini Moshi.
Nayo
Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida
kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani
Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume mjini Musoma.
Mjini
Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na
Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya
Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Leo
(Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza
na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za
marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
Timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya
Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15
na 16 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment