Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Takriban asilimia 30 ya watu 4,000 waliopoteza maisha kwa ajali za barabarani ni watembea kwa miguu .

 

Mrakibu wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Bonaventura Nsokolo akizungumza jambo na waandishi wa habari kuhusu siku ya usalama barabarani, kulia kwake ni Bw. Alpherio Nchimbi Afisa Mtendaji Mkuu wa Helmet Vaccine Initiative Tanzania.(Picha na Genofeva Matemu – MAELEZO).
Afisa Mpango Mwandamizi Bw. Peter Amos akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu wiki ya nenda kwa usalama barabarani itakayofanyika tarehe 11 Mei, 2013 katika shule ya Sekondari Turiani iliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam. (Picha na Immaculate Makilika – MAELEZO).
Na Elphace Marwa – MAELEZO.
Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na usalama barabarani AMEND Organisation kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani wameandaa matembezi mafupi ya kuukumbusha umma kuhusu hatari za barabarani wanazokabiliana nazo watembea kwa miguu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Afisa Mpango Mwandamizi wa AMEND Bw. Peter Amos amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2012 takribani watu wasiopungua elfu nne walipoteza maisha kwa ajali za barabarani ambapo asilimia 30 kati yao ni watembea kwa miguu.

Bw. Amos amesema kuwa matembezi hayo yatafanyika Jumamosi tarehe 11 mwezi Mei kuanzia saa tatu asubuhi katika shule ya Sekondari ya Turiani wilaya ya Kinondoni.
Aidha Amos amesema matembezi hayo yanalenga kuhamasisha watu kuchukua tahadhari wanapokuwa barabarani ili kulinda usalama wao na watembea kwa miguu.
Bw.Amos ameeleza kuwa jumla ya madereva 300 wa bodaboda wamepatiwa mafunzo na wameweza kufaulu vipimo vya udereva na kupatiwa leseni .
Kwa upande wake Mrakibu wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Bonaventura Nsokolo kutoka trafiki Makao makuu ametoa wito kwa waandishi wa habari kuelimisha jamii juu ya matumizi bora ya barabara kwani ajali za barabarani zimekuwa zikigharimu maisha ya watanzania wengi wasio na hatia.
Wakati huo huo Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Helmet Vaccine Initiative Tanzania Bw. Alpherio Nchimbi amesema taasisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine wana lengo la kupunguza kwa asilimia 50 vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kufikia mwaka 2020.
Wageni rasmi akiwemo Kamanda Mpinga wa Kikosi cha Usalama barabarani wanatarajiwa kuzungumza na wananchi siku hiyo ili kuwahamasisha kujilinda na ajali za barabarani na kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top