WAZIRI
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akikata utepe wakati wa
uzinduzi wa Kituo cha Umeme cha Kisutu Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto
ni Waziri wa Mambo ya Ulaya na Biashara ya Nje, Dk Alexander Stubb.
Na Mwamdishi Wetu
WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema
kuwa kunahitajika uwekezaji endelelevu katika sekta ya nishati na sio kutegemea
kuendelea kukopeshwa.
Muhongo alisema wakati uzinduzi wa Kituo cha Umeme
cha Kisutu Jijini Dar es Salaam ,alisema kuwa kuwekeza katika miradi ya umeme
kunaweza kuondokana na misaada na kuingia katika biashara makini .
Ujenzi wa Kituo hicho unatokana na Serikali ya Finland kutoa
msaada wa Bil.60 kwa ajili ya ujezi wa huo ambao utakuwa ni wa kisasa kwa
kuwaondolea usumbufu wafanyakazi wa Tanesco kwenda kutafuta sehemu yenye matatizo.
Muhongo alisema kuwa tangu mwaka 1961 bado Tanzania ni
masikini na ambapo sasa ni wakati wa kuwekeza katika miradi ambayo itatuondoa
katika kutegemea misaada.
Alisema mradi huo ni miaka mwili utasaidia kuondokana na
matatizo ya umeme katika maeneo ya mjini baada mradi kukamilika .
Waziri wa Finland wa
Mambo ya Nje ya Ulaya na Biashara Elexander Stubb alisema kuwa msaada
huo ni kutokana na ushirikiano mzuri baina nay a Finland na Tanzania.
Alisema kuwa wataendelea katika kusaidia katika nyanja
mbalimbali ili kuweza kupiga hatua ya kimaendeleo.
CREDITS: HABARIMSETO BLOG
Post a Comment