Msanii wa muziki wa kizazi kipya
ajulikanae kwa jina la Snura akiimba jukwaani wimbo wake unaotamba kwa
sasa katika vituo vingi vya redio,uitwao Majanga,mbele ya maelfu ya
watu waliofika kwenye uwanja wa Jamuhuiri jioni ya leo wakati wa kituo
cha redio ya Clouds FM ilipokuwa ikizindua msimu wake mpya kwa
wasikilizaji wake,uzinduzi huo ulikwenda sambamba na kufanyika kwa
semina ya fursa kwa Watanzania.
Msanii
mahiri wa Mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akiwakuna vilivyo wakazi wa
mji wa Dodoma jioni ya leo.alipowaangushia maneno kadhaa na umati
kulipukw ana mayowe kila kona,ambapo Clouds FM wamezindua msimu wao
mpya.
Maelfu ya Watu wakiwa ndani ya
uwanja wa jamuhuri jioni ya leo wakijumuika kwa pamoja na wana Clouds FM
walipokuwa wakizindua msimu wao mpya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya
a.k.a bongofleva katika miondoko ya Hip Hop,Izzo Bizziness akikamua kwa
shangwe kubwa mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika ndani
ya uwanja wa Jamuhuri,walipokwenda kushuhudia uzinduzi wa msimu mpya wa
Clouds FM.
Msanii wa muziki wa kizazi
kipya,Madee akitumbuiza mbele ya umati mkubwa wa watu ndani ya uwanja wa
jamuhuri,wakati wa kituo cha redio ya Clouds FM kilipokuwa kikizindua
msimu wake mpya.
Pichani shoto ni Mkurugenzi wa
vipindi na Utafiti,Ruge Mutahaba akizungumza na Katibu wa NEC,Itikadi na
Uenezi,Nape Nnauye ndani ya Uwanja wa Jamuhuri jioni ya leo,wakati
tamasha la uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM likiendelea,Nape alifika
uwanjani hapo kujionea shamrashamra mbalimbali zilizojumuisha maelfu ya
watu.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Aidha msimu huo umekwenda
sambamba na kaulimbiu inayofuatia harakati za MADE IN TANZANIA,ambapo
msukumo wake ni kuwashawishi Watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa
hizo kwa umoja wa maendeleo,huku neno TWENZETU likitumika kama neno
rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi uzinduzi huo utabeba harakati
rasmi za vita dhidi ya Uharamia wa kazi za wasanii,Wabunifu na wavumbuzi
mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.
mbalimbali.Kesho kutakuwepo na matembezi ya kampeni ya kupinda uharamia wa kazi za sanii yatakayoanzia uwanja wa Jamuhuri mapema asubuhi na kupolewa na Waziri Mkuu Mh. Pinda.








Post a Comment