NA MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA.
SERIKALI imesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF ) ni lazima kwa kila mtu ili kupunguza matatizo ya uhaba wa fedha kwa ajili ya matibabu huduma zaa afya.
Aidha ifafanua kuwa ifikapo mwaka 2015 bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itakuwa imefikia asilimia 15.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi wakati jana jioni mjini Dodoma ,alipokuwa akihitimisha mjadala wa kuhusu Makadrio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2013/2014 ya sh. 753,856,475,000 , kati ya fedha hizo sh. 282,573,534,000 ni kwa ajili ya mtumizi ya kawaida na sh. 471,282,941,000. ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Alisema serikali ina mpango wa kuongeza wigo wa huduma ya mfumo huo, hivyo utakuwa si hiari.
Alisema Serikali ina mpango wa kuwa na Sheria Mpya ya ‘National Social Health Insurance’, ambapo kila mtu atakuwa na bima hiyo ili kupunguza matatizo katika sekta ya afya.
Dk. Alisema lengo la serikali ni kupanua mfuko huo .
Akijibu hoja ya baadhi ya wabunge kuwa bajeti ya maendeleo inaonekana kuwa ni tegemezi ,Waziri huyo alisema ni kwa sababu wadau wa maendeleo wanaonesha kuchangia fedha nyingi katika eneo hio, hivyo fedha nyingi zinawekwa katika maeneo mengine.



Post a Comment