Mahmoud Ahmad
Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha
magessa Mulongo ameviwataka vyama vya wafanyakazi kuwachunguza waajiri wanao
kiuka sheria za kazi kwa kuajiri kwa miezi mitatu mitatu kwani wamekuwa
wakiwaacha wafanyakazi kama walivyowaajiri mwanzo bila ya mafao ya mwisho wa
kazi tuwakatae waajiri wasiofuta sheria za kazi natoa agizo kuanza kufanya
uchunguzi kwa waajiri kama hawa.
Kauli hiyo ameitoa kwenye
kilele cha siku ya wafanyakazi kwenye viwanja vya kumbu kumbu ya Sheikh Amri
Abeid jijini hapa na kusema kuwa wapo waajiri wa aina hiyo wengi wasiojali
maslahi ya wafanyakazi na mwisho wa siku kuwaacha hawana mafao yeyote huko ni
kuwaumiza wafanyakazi.
Mulongo alisema kuwa
kumekuwapo na wahitimu ambao wenye stashahada na Diploma wamekuwa wakiongoza kwa
utendaji mzuri wa kazi wakati wenye digrii wakiwa hawana uzoefu na moyo
wakuifanyakazi na kubaki kupiga fitna na wakati wakiwa vyuoni walikuwa
wakifuatilia siasa na kuacha kufuta taaluma zilizowapeleka vyuoni
humo.
“Ndugu zangu wafanyakazi
wenzangu Taaluma yeyote inahitaji muda mzuri wa kuifuatilia tangu ukiwa chuoni
hadi unaingia kazini sasa hapa upo chuoni unaacha taaluma unafuata mambo yasio
ya taaluma huku ni kutokuwa na wataalamu wa kufaa hapo ndipo fitna
zinapoanzia”alisema Mulongo.
Mulongo alienda mbali na
kuwataka wanahabari kuandika habari kufuatana na taaluma zao na kuacha ushabiki
wa kisiasa kwani taaluma ya uandishi wa habari ni taaluma yenye weledi na ina
miiko na maadili hapa ndugu zangu tuelimishe jamii masuala ya kimaendeleo badala
ya kijikita kwenye masuala ya kisiasa zaidi na kuicha nchi ikielekea kwenye
lingi la vurugu.
“ipo wakati mtajikuta
mkiangukia kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma mbali mbali kwani mtakuwa
mmeacha taaluma na kuuvaa ushabiki wa kisiasa hapo mtakuwa hamuitakii nchini
yenu maendeleo bali mtakuwa mnaitakia nchi yenu mabaya”alisema mkuu wa
mkoa.
Sherehe hizo zilienda
sambamba na maandamano ya vyama vya wafanyakazi na makampuni mbali mbali huku
maonyesho ya magari yakitia for a hasa kampuni ya Megatrade Investment
watengenezaji wa Kiroba orgin na Kvant Gin na Kiwanda cha Banana Ivestment Huku
kwenye viwanda vya kutengeneza nguo Kampuni ya AtoZ ikitia for a ikifuatiwa na
kampuni ya Sunflag zote za jijini
hapa
Post a Comment