*Utafiti wabaini ina kiwango kikubwa cha kemikali hatari mwilini mwa binadamu
AFYA za
mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo
hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za
sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.
Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti
huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya
soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi
ya binadamu.
IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Post a Comment