MBUNGE
wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa
amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.
Ndasa
aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu
kurushwa katika sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya
watu wawili na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.
“Mheshimiwa
Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana
hofu ya kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa
hafifu,” alisema Ndasa.
Ndasa
alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha
hivyo ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara
makubwa kwa taifa.
Wabunge leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.
Post a Comment