NA MAGRETH KINABO – MAELEZO, DODOMA
BUNGE
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeazimia kuitaka Serikali
kuchukua mara moja dhidi ya viashara vya aina yoyote ya uvunjifu wa
amani unaojitokeza ilikuwapa wananchi matumaini ya kujumuika na kubudu
kwa uhuru bila kuwa na hofu ya usalama wao.
Azimio
hilo limepitishwa leo Bungeni kufuatia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah alipowasilisha Azimio la Bunge la
Kulaani Tukio la Kulipuliwa kwa Bomu katika Kanisa la Katoliki la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, jijini Arusha , Mei
5,mwaka huu.
“Pamoja
na kazi nzuri iliyokwishafanywa na Serikali ya kuwakamata baadhi ya
watuhumiwa, Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kwa kuzingatia majukumu
yake ya msingi kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili,
mwaka 2013, Kanuni ya 118 ikisomwa pamoja na nyongeza na Nane, Kifungu
cha 6(3),.
“Inaomba kuleta azimio la kuitka Serikali na vyombo vyote vya ulinzi na
usalama kuhakikisha kuwa inatumia uwezo wake wote kuendeleza uchunguzi
wa kina na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hili kubwa na
la kinyama na kuwafikisha katika vyombo vya sheria haraka iwezakanavyo
ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao,” alisisitiza.
Akichangia azimio hilo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini-CHADEMA
Kabwe Zitto alisema tunaweza kuwa na sheria ya kupiga marufuku lugha za
uchochezi kwa Watanzania zinazoweza kuligawa Taifa.
“Mikanda
inauzwa hadharani inawagawa Watanzania tunaomba kipengele hiki kamati
iingize katika azimio wanasheria watatusaidia,” alisema Zitto.
Mbunge
wa Jimbo la Kibakwe – CCM George Simbachawene alisema; “inaweza kuwa
ni fursa na kauli zetu tunazotoa kama viongozi wa dini au kisiasa kwa
wengine tunawapelekea ujumbe inakuwa ni mapambano”, .
Kwa upande wake James Mbatia – NCCR Mageuzi aliiomba Serikali isimamie sheria zilizopo.
“Wanasiasa
tuna mkono wetu mkubwa kwa yeyote ni wajibu wetu sote usitake kupata
maradaka kwa kumwaga damu ya Watanzania. Nawaomba Watanzania tuwe kitu
kimoja,” alisema Mbatia .
Naye Mbunge Jimbo la Vunjo –TPL Agustino Mrema alitaka jamabo linapotokea hatua zichukuliwe mara moja.
Aliongeza
kuwa wahubiri wanaopewa kibali cha kuhubiri na wanatukana na kutoa
lugha za uchochezi, vikundi au madhehebu vichukuliwe hatau, ambapo
alitoa siku saba.
Mbunge wa Viti Maalum – CCM Getrude Rwakatare aliomba viongozi wa dini kuhuri upendo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaratibu , Stephen Wassira, ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Bunda – CCM ,aliwashauri wabunge kuungana
pamoja ili kushinda tatizo hilo.
“
Waliopatikana watatusaidia Serikali , hakuna atakayepona Serikali
itachukua hatua. Tunaendelea na kazi hiyo hadi nchi inakuwa na amani,”
alisema Waziri Wassira.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo alisema suala la kupitia sheria ni la msingi na kamati
hiyo italiangalia. Pia aliongeza hata lugha ya uchochezi hata Bungeni
hairuhusiwi kwa pande zote.
“Jambo hili halifai tumeanzisha sisi humu ndani wimbo watu wanaitikia. Lazima tuilinde nchi kwa udi na uvumba.
”Hakuna kiongozi atakayechaguliwa kwa udini nchi hii lazima achaguliwe na Wakristo na Waislamu,” alisema.
Spika wa Bunge hilo, Anne Makinda aliwataka wabunge kuchunga kauli zao.
Katika
hatua nyingine spika huyo aliondoka kwenda Arusha kwa safari ya siku
moja na baadhi wa wabunge ili kutoa pole kwa wananchi wa Arusha.
Post a Comment