TIMU ya Yanga leo imetimkia Visiwani
pemba kwa ajili ya kuanza kambi yao ya kujiwinda na mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom dhi ya watani wao wa jadi Simba, mchezo utakaopigwa Mei 18
kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Wakati Kambi hiyo ikianza leo, Wazee wa
klabu ya yanga wametoa tamko juu ya mchezo wa marudiano na watani wao,
ambapo wazee hao walianza kutoa pongezi kwa Viongozi wa Klabu ya YANGA
chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu Mwenyekiti Clement Sanga kwa
kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu
huu wa mwaka 2012/2013.
Akizungumza
kwa niamba ya wazee wenzake Ibrahim Akilimali amesema ubingwa wa
yanga umetokana na Uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu
ya Klabu na kufikia malengo.
Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya Uongozi, wanachama na wachezaji wetu.Hivyo
basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na wachezaji
wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na
Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe
na nderemo.
Sherehe haitakuwepo kama watashindwa kumfunga myama mei 18 uwanja wa taifa
Credits: Sufiani Mafoto



Post a Comment