Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Inguun Klepsvik Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar na kuiomba Norway kuangalia uwezekano wa kusaidia utaalamu wa Uvuvi wa Bahari Kuu.
**************
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amekutana kwa mazungumnzo na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn Klepsvik ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliiomba Norway kuangalia uwezekano wa kuisadia Zanzibar kitaaluma katika sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu kwa vile Nchi hiyo imepiga hatua kubwa katika eneo hilo.
Amesema Zanzibar imezungukwa na bahari pembe zote, rasilmali ambayo ikitumika vyema inaweza kusaidia kutoa ajira kwa kiwango kikubwa zaidi na kusaidia pia uchumi wa Taifa sambamba na kupunguza umaskini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemueleza Balozi huyo wa Norway Nchini Tanzania kwamba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika azma yake ya kuimarisha uchumi, sekta ya Uvuvi imepewa msukumo na kinachoangaliwa zaidi wakati huu ni kuwashawishi washirika wa Maendeleo na Nchi hisani kuunga mkono sekta hiyo.
Aliipongeza Norway kwa juhudi zake za kuendelea kuunga mkono harakati za maendeleo za Zanzibar kupitia Shirika lake la Maendeleo la Norad ambapo Zanzibar tayari inaendelea kufaidika na sekta za nishati na mawasiliano ya barabara kutokana na mchango wa Taifa hilo Hisani.
Naye Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bibi Ingunn Klepsvik amemuhakikishia Balozi Seif kwamba Nchi yake itahakikisha kwamba sekta zilizopata msaada wa Nchini hiyo zitaendelea kuungwa mkono zaidi.
Balozi Ingunn amezitaja baadhi ya sekta zilizoungwa mkono na Serikali yake visiwani Zanzibar kuwa ni pamoja na Sekta ya mawasiliano ya Barabara Kisiwani Pemba pamoja na Sekta ya Nishati Vijijini.
Post a Comment