Na Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry
MWILI
wa mshambuliji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, Abdallah Msamba
aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi, Dar es
Salaam unatarajiwa kuzikwa kesho makaburi ya Magomeni Makuti Jijini.
Kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Simba SC, Madaraka Suleiman ‘Mzee wa Kimyinio’, mwili wa marehemu kwa sasa upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya JWTZ, Lugalo, Dar es Salaam.
Madaraka alisema mwili huo utarejeshwa nyumbani kwake Mbezi kwa ajili ya zoezi la ibada na kuagwa kesho kabla ya kupelekwa Magomeni kwa mazishi.
“Na ratiba hii imepangwa na baba wa marehemu mwenyewe ambaye tulikuwa naye msibani leo, kwa hivyo naomba wapenzi wa soka kesho waje tushiriki zoezi la kumuaga ndugu yetu na kipenzi chetu, Msamba,”alisema Madaraka.
Msamba ni mmoja kati ya washambuliaji bora wa pembeni kuwahi kutokea Tanzania ambaye alikuwa ana nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kufunga mabao.
Kisoka aliibukia Pan African pamoja na akina Bakari Malima, Thomas Mashalla, Ally Yussuf ‘Tigana’ na wengineo kabla ya kuhamia Sigara na baadaye Simba SC kisha kumalizia soka yake Kajumulo WS.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

Post a Comment