Mshitakiwa Isambi Mwazembe muda mfupi baada ya Mahakama kutupilia mbali kesi yake ya ubakaji
Mshitakiwa Isambi Mwazembe akiwa haamini kama kesi yake imeisha
Mshitakiwa Isambi Mwazembe akiwa mwenye Furaha baada ya kesi yake kwisha
Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imemwachia huru Mshitakiwa wa
kosa la ubakaji aliyekuwa amehukumiwa kutumikia kifungo cha miak 30 na Mahakama
ya Wilaya.
Mtuhumiwa huyo Isambi Mwazembe (29) alidaiwa kutenda kosa
hilo Mwaka 2003 ambapo baada ya kukutwa na hatia alihukumiwa kifungo hicho
kasha kutumikia kifungo miaka minne kabla ya Mahakama kuu kumwachia huru baada
ya kukata rufaa.
Akipitia rufaa iliyoletwa mahakamani hapo Jaji Atuganile
Ngwala amesema sababu kubw iliyosababisha atengue kifungo hicho ni kipengele
kilichotumiwa na mahakama ya chini kuwa hakikufanywa kisheria.
Amesema kipengele kilichotumika ni kwamba Mahakama hiyo
ilipokea PF 3 kutoka kwa mhanga wa kosa ilo badala ya kupokea kutoka kwa
Daktari aliyemfayia vipimo kama
kielelezo.
Pia amesema katika maelezo ya daktari yanadai binti huyo
kubakwa baada ya kukutwa na michubuko na damu sehemu zake za siri licha ya
kumkuta na Bikra kitendo lichodai kuwa sentensi hiyo haikuwa na uhkika.
PICHA NA MBEYA YETU
Post a Comment