Mbunge wa kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli
Habari zilizoifikia Maisha Times muda huu kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la, tukio hilo limetokea jioni hii wakati Mh. Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Mh. Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.
Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.
Maisha Times itazidi kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tukio hili kadiri habari zitakavyozidi kupatikana.
Post a Comment