Mgombea
wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana ameibuka mshindi wa
uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mianzini uliofanyika jana kwa
kupata kura 1283, huku Mgombea wa Cuf akipata kura 494, Chadema
wakiambulia kura 315 na ADC walipata kura 26, NRA kura 9 na Mgombea wa
NCCR Mageuzi akiambulia kura 1. Bawji amemzidi mshindi wa pili kwa zaidi
ya nusu ya kura.
Mara
baada ya matokeo kutangazwa na tume kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata,
Wanachama wa CCM waliletewa matokeo yale na kusomwa na Mkurugenzi wa
uchaguzi wao ambaye ni Katibu kata wa Mianzini wa CCM, Abdallah Kihuku
mbele ya hadhara ya Wana CCM waliofurika katika ofisi za kata . Picha na
Emmanuel Shilatu wa http//: www.ndgshilatu.blogspot.com
Mshindi
mteule wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana akiongea
machache kwa Wana CCM mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi. Bawji
anaziba nafasi iliyokuwa wazi kufuatia kifo cha diwani wa kata hiyo.
Mwenyekiti
wa Mkoa wa CCM, Ramadhan Madabida akiwashukuru wana CCM kwa umoja na
mapambano ya dhati yaliyopelekea ushindi wa CCM. Huu ndio uchaguzi wake
wa kwanza tangu awe Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni uchaguzi
mdogo wa pekee wa udiwani kwa Mkoa wa Dar Es salaam.
Katibu wa Mkoa wa CCM, Abdillah Mihewa naye pia akitoa yake ya moyoni.
Katibu wa Wilaya ya Temeke wa CCM, Ndg Robert Kihaka akiwashukuru Wana CCM kwa uvumilivu wao na jitihada zao zilizozaa matunda mema.
Mida ya jioni, tayari wana CCM walishaanza heke heka za kushangilia ushindi.
Mjumbe
wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John akiwasili toka
kuwakusanya mawakala wa CCm kwenye vituo vyao vya kupigia kura.
Wana CCM walifurika katika ofisi za kata ya Mianzini wakishangilia ushindi. Ilikuwa ni raha tupu.
Post a Comment