BEI za mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa zimepungua kwa tofauti ya
sh 16 na 72 kwa lita ikilinganishwa na mwezi uliopita.
Taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi na Injinia Mutaekulwa Mutegeki
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) ilisema kila mwezi
mamlaka hiyo imekuwa ikitangaza bei kikomo na elekezi ili kudhibiti upandaji
holela wa bei kwa mafuta.
Ilibainisha kuwa bei hizo zimeanza kutumika jana na mafuta ya petroli
yamepungua sh 16 kwa lita sawa na asilimia 0.76; dizeli sh 42 sawa na asilimia
2.16 na mafuta ya taa kwa sh 72 sawa na asilimia 3.50.
Taarifa hiyo ilibainisha bei za bidhaa za mafuta zitaendelea kupangwa na
soko, huku Ewura itashiriki kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei
kikomo za bidhaa za mafuta.
Iliongeza kuwa mabadiliko hayo ya bei yametokana na bei za mafuta katika soko
la dunia sambamba na sheria ya mafuta ya mwaka 2008.
Taarifa hiyo iliweka wazi kuwa kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za
mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi ziko chini ya bei kikomo kama
ilivyokokotolewa na kanunimpya iliyopitishwa na Ewura mwaka 2011 .
Wakati huo huo, vituo vyote vya mafuta vimetakiwa kuchapisha na kuonyesha
bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionyesha bei ya
mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo
husika.
Mkurugenzi huyo mkuu aliwatahadharisha wamiliki wa vituo vya mafuta kuwa ni
kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na
adhabu itatolewa kwa kituo husika.
TANZANIA DAIMA
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
Alfajiri12 hours ago
-
-
-
-
-
-
Serikali yatoa kauli kuhusu Dbi ya Kariakoo9 months ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-


Post a Comment