CHAMA cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kutoa tamko kuhusu rasimu ya
mabadiliko ya Katiba iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Akizungumza
na Tanzania Daima jana Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri wa CHADEMA John Mrema
alisema kwa sasa viongozi wa juu na watalaamu wanaisoma na
kuichambua.
“Hatuwezi
kutoa maoni ya juu juu kuhusu rasimu ya katiba… ni kitu nyeti ambacho kinatakiwa
kufanyiwa kazi kwanza ili chama kitakapozungumzwa iwe kwa ajili ya manufaa ya
Watanzania wote na si ya mtu mmoja ndiyo maana kazi hii tumeikabidhi kwa
wataalam,” alisema Mrema.
Pamoja na
mambo mengi wachambuzi hao watapitia mambo yaliyokubaliwa na yaliyoachwa ili
kuionyesha tume hiyo kuwa kuna ambayo yana manufaa kwa taifa ingawa
wameyaacha.
Katika
rasimu hiyo mambo yaliyoachwa ni pamoja na serikali ya majimbo kwa sababu kuwa
gharama za kuiendeshea zitaongezeka endapo serikali tatu zitakuwapo pamoja
kuweza kufumuka mambo ya udini, malalamiko, dalili za kujitenga, ukabila na
ukanda.
Mambo
mengine yaliyokataliwa katika serikali ya muungano ni Mahakama ya Kadhi kwa
maelezo kwamba nchi washirika zinaweza kulijadili.


Post a Comment