Miss Tabata Dorice akipozi
na Mshindi wa pili Upendo Lema (kulia) na Mshindi wa tatu Recho Mushi
(kushoto).
|
Na
Mwandishi Wetu
Mwamafunzi
wa mwaka wa pili katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere Dorice Mollel
(22) usiku wa kuamkia jana alishinda taji la Miss Tabata kwenye shindano
lililofanyika katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata.
Dorice
aliwabwaga warembo
wengine 14 kumrithi Noela Michael aliyekuwa anashikilia taji hilo. Noela ndiye
anayeshikilia taji la Miss Ilala kwa sasa.
Mshindi
huyo alizawadiwa Sh 600,000 na king’amuzi kutoka Multichoice pamoja na warembo
waliyoshika tano za juu watawakilisha Tabata katika shindano la Miss Ilala
baadaye mwaka huu.
Warembo
hao ni Upendo Lema (22) aliyezawadiwa sh 400,000 baada ya kushika nafasi ya pili
na Recho Mushi (20) alipata Sh 300,000 baada ya kushika nafasi ya tatu. Wengine ni Kazunde
Kitereja (19) alishinda nafasi ya nne na kuzawadiwa Sh 200,000 na Kabula Juma Kibogoti (20)
alipataSh 150, 000 kwa kushika nafasi ya tano.
Warembo wengine waliyoingia kumi
bora kila moja alipata shilingi laki moja. Nao ni Madgalena Bhoke
(21), Eunice Nkoha
(19), Rehema Kihinja (20), Brath Chambia (23) na Joaniter Kabunga (21). Warembo
waliyosalia walipata kifuta The rest got consolation prize of Sh 50,000
each.
Miss
Tabata iliandaliwa na Bob Entertainments na Keen Arts chini ya udhamini wa Dodoma Wine, Redd’s Original,
Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated
Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Post a Comment