Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ELIKANA, ELIUD: WATOTO WALIOUNGANA WANAOTUMIA NJIA MOJA KUJISAIDIA: KUPELEKWA INDIA KUFANYIWA UPASUAJI WA KUWATENGANISHA

 


Na Vicky Kimaro, Mwananchi
Dar es Salaam. “Madaktari waliponiambia kuwa watoto wangu wameungana nilichanganyikiwa, niliona dunia imenigeuka, sikuwahi kuwaza nitakutana na kitu cha namna hii katika maisha yangu.”
Ni maneno ya binti kutoka kabila la Wandali ambalo asili yake ni Mbeya, Grace Joel (19), ambaye Februari 20 mwaka huu, alijifungua mapacha wa kiume ambao wameungana katika sehemu ya kiunoni.
Mwanadada huyo anasema hakuamini macho yake pale madaktari wa Hospitali ya Uyole iliyopo mkoani humo walipomwambia kuwa watoto wake wameungana na hivyo kupewa rufaa ya kwenda kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa wa Mbeya.
"Wakati wa ujauzito wangu sikuwahi hata siku moja kuhisi kuwa ningeweza kuzaa watoto wakiwa kwenye tatizo hili, sikuwahi kuumwa zaidi ya kuvimba miguu tu na  hiyo ni hali ya kawaida kwa mjamzito yeyote." anasema Grace ambaye kwa sasa anahitaji msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha ya watoto wake.
Licha ya umri huo mdogo, amejikuta kwenye hali ya mateso na uchungu mwingi baada ya familia yake, hususani mume wake, Erick Mwakyusa kumtelekeza kwa kile alichodai kuwa hana haja na watoto walioungana.
Kwa msaada ili kuokoa maisha ya 
watoto hawa piga namba 

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top