Mwenyekiti
wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani
akiwatambulisha watoto yatima Irene Joachim Katikati na Geofrey Yohana
watakaopanda mlima Kilimanjaro katika kuhamasisha taasisi na mashirika
mbalimbali kuchangia fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi
nchini Tanzania hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine.
Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma Mrisho,
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee
Mark Bomani na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar
Issa wakimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni
15,000,000 Sister Adalbera Mukure wa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea
watoto yatima cha Moyo wa Huruma cha Geita wakati wa hafla maalum ya
kukabidhi fedha hizo kwa mashirika mablimbali yanayopambana na ugonjwa
wa ukimwi iliyofanyika Ijumaa kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini
Dar es salaam fedha hizo zinakusanywa Mgodi wa Dhahabu ya Geita Gold
Mine na washirika wake kwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar
Issa, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti
Mzee Mark Bomani na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma
Mrisho, wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa TACAIDS kutoka
kulia ni Jumanne Issango Mkurugenzi wa Uraghibishi, Beng’i Issa
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na Moriss Lekule Mkurugenzi wa Mwitikio
wa Taifa hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine.
Mgodi
wa Geita kujiandaa na mwaka mwingine wa Kilimanjaro Challenge katika
Hotel ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, Tanzania Ijumaa
iliyopita. Pia ufunguzi wa hafla huo ulihusisha kutaja majina ya asasi
zitakazo faidika na fedha zilizokusanywa katika upandaji mlima mnamo
mwaka wa 2012.
Mpango
huu kwa mara ya kwanza ulianzishwa mnamo mwaka 2002 ukihusisha
wapandaji mlima 47 uliowezesha kukusanya kiasi cha fedha za kitanzania
milioni 62. Ni mafanikio hayo yaliyoipa nguvu na moyo Geita Gold Mine
kufanya tukio hilo la upandaji mlima kama tukio la kitaifa la kila
mwaka. Tangu wakati huo wastani wa wapandaji 50 mpaka 55 walijiunga na
msafara huo kila mwaka. Hadi sasa, zaidi ya watu 500 kutoka duniani kote
wameshiriiki katika kukusanya zaidi ya fedha za Kitanzania Billioni 2
ambazo zimenufaisha zaidi ya asasi zisizo za kiserikali 30 NGO nchi
nzima katika kupambana na VVU/UKIMWI Tanzania.
“Lengo
la Kilimanjaro Challenge ni kujenga uelewa zaidi juu ya janga la
VVU/UKIMWI, kutoa msaada wa kifedha kwenye mpango huo na kujenga timu
bora ya kitaifa katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI.” Alisema Bwn.
Godvictor Lyimo
Mpango
huu wa kujitolea na ule wa serikali unawapa nafasi wapandaji wa ndani
kupanda mlima Kimlimanjaro. Katika miaka 11 iliyopita watu wengi
wameshiriki katika kupanda mlima kwa kujitolea,akiwemo mvulana wa miaka
11 na mzee wa miaka 84, Raisi wetu Mstaafu Mhe. Mzee Ali Hassan
Mwinyi. Kwa mujibu wa Waziri mkuu Mhe. Mizengo K. Pinda, uamuzi
uliofanywa na Mzee Mwinyi ulikuwa ni wa kujidhatiti, akinukuu kauli ya
‘Mbiu ya Mgambo’ katika uamuzi huo.
Kwa
mujibu wa Bwn Godvictor Lyimo Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani GGM,
“Imeripotiwa kwamba kiwango cha maambukizi kimepungua kutoka asilimia 13
mwaka 2000 hadi asilimia 7.8 mwaka 2007 na kwenda chini zaidi mpaka
asilimia 5.1 mwaka huu 2013. Kama moja ya jitihada za kuongeza uelewa
juu ya VVU/UKIMWI, Raisi Jakaya Kikwete alizindua kampeni ya upimaji wa
hiyari wa VVU/UKIMWI kwa kutumia mwamvuli wa “Kilimanjaro Challenge” GGM
mpango huu umepata mafanikio katika kutoa uelewa juu ya janga hili na
tunaangazia kuendeleza jitihada hizi mpaka pale Tanzania itakapo tangaza
kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ni sifuri.”





Post a Comment