Mwanamke Mery Mbosa anayeishi kama mkimbizi baada
ya kunusurika mara kadhaa kuchinjwa na mtalaka wake.
------------------------------------------------------------
Na Gustav Chahe,
Iringa
MAMA mmoja mkazi wa Itunundu – Pawaga katika Mkoa
wa Iringa Mery Mbosa anaishi kama digidigi baada ya kunusurika mara kadhaa
kuchinjwa na mtalaka wake na kulazimika kuhama kijiji kwa ajili ya kunusuru
maisha.
Akiongea na mtandao huu jana, Bi Mbosa alisema
maisha yake yapo hatarini kutokana na kuvamiwa na mtalaka wake mara kadhaa akiwa
nyumbani na kumuumiza.
Alisema alilazimika kutalakiana baada ya
mwanamume huyo kuwa mkorofi kiasi cha kupigwa, kutokuwa huru kutumia mazao
ambayo walilima wote na hata kutokuwa huru kuongea na watu hata kama ni ndugu
zake kwa madai kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Alisema mtalaka wake amegeuka kuwa mnyama na
kufika nyumbani kwake usiku wa manane na pindi anapokuta mlango umefungwa huanza
kurusha mawe madirishani huku akitaka kuvunja mlango ili kuingia
kumdhuru.
Amemtaja mtalaka wake kuwa ni Phabiani
Msilamgunda ambaye miezi ya hivi karibuni alikutana na ye njiani akielekea
shambani akamvamia akiwa na kisu kwa kutaka kumchinja na kuokolewa na watu ambao
walikuwa jirani.
“Ilikuwa 23 Machi mwaka huu nilikuwa nikielekea
shambani nikakutana na mtalaka wangu akiwa na kisu mkononi akanivamia huku
akisema nakuchinja laeo lakini kwa bahati nzuri kulikuwa na watu jirani
wakaniokoa vinginevyo ningekuwa marehemu.
“Lakini hata hivyo amekuwa akimtukana hata mama
yangu mzazi (mama mkwe) akitaka kupiga pia na kila wakati nimekuwa nikishtaki
hadi ofisi zinanichoka pamoja na kuwa ninapokelewa na akiitwa haendi kwa sababu
amekuwa mbabe” alisema bi Mbosa.
Hata hivyo Mbosa alisema kuwa aliwahi kupigwa na
kuumizwa vibaya na kulazimika kushtaki mahakamani japo kuwa hukumu ilivyotolewa
haikuwa ya haki na kuhatarisha zaidi maisha
yake.
“Nilipigwa na kuumizwa vibaya kesi ikapelekwa
mahakamani lakini hukumu ilivyotolewa haikuwa ya haki kwangu na baada ya hukumu
maisha yangu yamekuwa ni ya hatari zaidi” alisema.
Kwa mujibu wa maelezo ya wananchi wa kijiji hicho
ambao wameeleza kushuhudia mama huyo akinusurika kuuawa na jinsi maisha yake
yanavyozidi kuwa mabaya, walisema kiburi cha Msilamgunda kinatokana na dada yake
ambaye ni diwani wa viti maalum (CCM).
Gazeti hili limebaini kesi ambayo mama huyo
hajaridhika na hukumu ni Jinai No. 22/2013, mshitakiwa Phabiani Msilamgunda
ambayo ilitolewa hukumu Mei 21 Mwaka huu.
Imeelezwa kuwa katika utoaji huku hiyo hakimu
aliyetajwa kwa jina moja la Masuwe alimtaka mtuhumiwa alipoe faini ya shilingi
laki mbili pamoja na gharama ya kesi shilingi 45 elfu jambo ambalo lilifanyika
hivyo na mtuhuhumiwa kuwa huru kwa vitisho kuwa lazima ammalize mwanamke
huyo.
Pamoja na kutokuridhika na hukumu iliyotolewa,
Mkuu wa kituo cha Polisi cha Pawaga Fedrick Nyavilwe anatuhumiwa kumdhurumu mama
huyo na kuiomba serikali kumsaidia ili aishi kama wanavyoishi wananchi
wengine.
Nyavilwe anatuhumiwa kumdhurumu mwanamke huyo
mbegu ya mpunga na kumfanya kuwa mtumwa kwa kukosa chakula bila kujua hatima ya
maisha yake.
“Baada ya hukumu nilikwenda shambani nilikokuwa
ninaanda mbegu ya mpunga kwa ajili ya kupanda nikakuta watu wananing’oa,
nilipouliza walisema wametumwa na Mkuu wa kituo cha polisi. Hivi sasa naishi
kama ndege jamani sijui nitakula nini kwa sababu hata mashamba niliyokuwa nalima
nilinyang’anywa na mbegu niliyokuwa nimeandaa kwa ajili ya kupanda polisi
wameninyang’anya” alisema.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kwa ajili ya
kutolea maelezo, Veronica Msilamgunda ambaye ni ndugu na Phabian Msilamgunda
alisema hawezi kuzungumza chochote kwa kuwa yupo kwenye
mkutano.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph
Malinga alipotafutwa kwa ajili ya ufafanuzi Alikiri kuwa mama huyo ni mhanga
mkubwa na anaishi kama mkimbizi kwa hofu ya kuuawa.
“Nalijua sana hilo na ninashukuru kwa kuwa
umenitafuta ili nikueleze. Maisha ya huyo mama hatuji yataishia wapi kwa sababu
hali ilivyo kwa sasa ni ngumu na anaishi kama
mkimbizi.
“Hata akiwa sehemu yenye ulinzi anaona kama
hakuna ulinzi kwa sababu ya kile anchofanyiwa. Kiujumla hata sisi viongozi wa
kijiji tunaishi kwa mashaka kwa sababu tunatishiwa kuuawa tunapotaka kutafutas
suluhu ya huyo mama. Huyu mwanaume tunashindwea kuelewa kama ni mtu wa kawaida
maana amegeuka kuwa kamas samba” alismea Malinga.
Hata hivyo alisema anaomba kwa watu wanaoweza
kumsaidia mama huyo kupata hifadhi ili aondokane na maisha ya kuishi kama
digidigi kule kijijini.
Chanzao:mbondelewis.blogspot.com
Post a Comment