 |
| Naibu
katibu mkuu wa CCM Tanzania bara akiwasili viwanja vya kata ya
kaloleni-stendi jioni ya leo kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kampeni
za uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya kaloleni Jijini Arusha |
 |
| Naibu katibu Mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akilakiwa na Bibi mwanachama wa CCM eneo la mkutano kaloleni jijini Arusha |
 |
| Naibu
katibu mkuu wa CCM Mh.mwigulu Nchemba akilakiwa na mgombea UDiwani wa
kata ya kaloleni kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Thomas |
 |
| Naibu
katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akisaini kitabu cha wageni baada
ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara kwaajili ya kampeni za uchaguzi wa
Udiwani kata ya kaloleni jijini Arusha |
 |
| CCM
inalea na kukuza watoto kwaajili ya taifa lenye Heshima na ustaarabu
siku za Usoni.Hawa na Vijana wa CCM wakisoma ngonjera mbele ya naibu
katibu mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba |
 |
| Kushoto
ni aliyekuwa diwani wa CHADEMA Ndugu Rehema sasa ni kada mtiifu wa
CCM.Kulia ni Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM ndugu Emmanuel Thomas |
 |
| Aliyekuwa
diwani wa CHADEMA Ndugu Rehema akisalimia wananchi na kuwaomba waachane
na CHADEMA ili wapate maendeleo kuanzia ngazi ya kata hadi wilaya na
Kitaifa.Amesisitiza CHADEMA ni chama cha watu wachache na chenye mlengo
wa maslahi binafsi.Amewaomba wanaarusha kuchana na adha ya kuamrishwa
kila kitu na Mbunge wao wa maandamano Ndugu Godbless Lema.Amesema yeye
ameshakaa chadema na anajua uchafu wote unaofanyika kuanzia kwa
Mwenyekiti wa chama,katibu mkuu wa chama na hata ngazi za chini.Hivyo
amewaomba wanaarusha kumchagua diwani wa CCM kwa maendeleo ya kata ya
kaloleni |
 |
| Kada
wa CCM Bi.Juliana Shonza akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza
kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi kata ya Kaloleni.Bi.Juliana shonza
amewaomba wakaloleni na Wanaarusha kuacha kutumika,Kuacha kuwa wafusai
wa mtu,Kuacha kuliangamiza jiji la arusha kiuchumi kwa kuendelea
kuikumbatia CHADEMA.Amesisitiza yeye alikuwa chadema na alikuwa kiongozi
wa juu ndani ya chama ameona namna chama kinavyoendeshwa kwa maslahi ya
watu wachache.Hivyo chaguo sahihi kwa wanakaloleni na wanaarusha ni
kuipa nafasi CCM kwenye uchaguzi huu wa Udiwani |
 |
| Bi.Juliana
shonza akisisitiza kwamba hakuna chama kama CCM,CCM ni chama chenye
mlengo wa kitaifa kimaendeleo.CCM ni chama tawala na kinamaslahi jamii |
 |
| Kada
wa CCM na aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la mbozi Mashariki kwa tiketi
ya CHADEMA kabla hajachukua uamuzi wa kujiunga na CCM Ndugu Mtela Allam
mwampamba akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya kaloleni jijini Arusha.Mtela
Mwampamba amewaomba wanaarusha kumpatia elimu mbunge wao kuhusu
mahusiano kati ya maendeleo na serikali iliyopo madarakani.Amesema
Mbunge w Arusha mjii Godbless Lema hajui maana ya maendeleo na
serikali,anafanyakazi kubwa ya kutenganisha maendeleo ya Arusha na
serikali.Amesisitiza Lema si mwanasiasa bali ni binadamu aliyezoea
maisha ya kihuni ndio maana siku zote anatafuta wahuni wenzake
ilikuivuruga Arusha.Ameomba wanakaloleni kumpigia kura Diwani mtarajiwa
wa CCM Ndugu Emmanuel Thomas |
 |
| Hapa
kada wa CCM mtela Mwampamba akiwahoji wanakaloleni kwamba yeye amekuwa
chadema tena mgombea ubunge mwaka 2010 na kupata kura 32000 jimboni
kwake Mbozi,lakini kwa kuchunguza mwenendo wa CHADEMA na kutambua ni
chama cha watu wachache wenye maslahi yao akaamua kujiunga na CCM chama
chenye mlengo wa kitaifa.Je wanakaloleni mimi mwampamba ninakura 32000
lakini nimeachana na chama cha maandamano,je wewe kijana unayenyweshwa
viroba siku za maandamano na hata huyo Mbowe hakujui unanufaika na nini
na CHADEMA? |
 |
| Mtela
Mwamapmba akihutubia mamia ya wananchi na wakazi wa kaloleni jioni ya
leo tar.8/06/2013.Amewaomba wanakaloleni kumpa kura mgombea wa CCM kwa
sababu chadema wanafukuza madiwani bila sababu na kulitia hasara
taifa.Pia CHADEMA hawanachakutekeleza zaidi ya kuandaaa maandamano na
vurugu ndani ya jiji la Arusha. |
 |
| Huyu
kijana alikuwa kamanda wa CHADEMA,amesema aliachana na CHADEMA baad aya
kugundua kuwa anapoteza muda wake kuhangaikia watu binafsi na sio
maslahi jamii.hapa alikuwa anaonesha barua na hati mbalimbali
anazofanyia utapeli Mbunge wa Arusha mjini Ndugu GodBless Lema.Ameeleza
namna Lema alivyoweka ARUSHA DEVELOPMENT FOUNDATION mali ya familia
yake,Mke wa Godbless lema ndiye Mkurugenzi wa mfuko huo.Hivyo amewasihi
vijana wenzake kuachana na CHADEMA,Wafanye chaguo sahihi kwa kumpa kura
mgombea wa CCM |
 |
| Mh.Munge
Devotha Likokola akihutubia mamia ya wananchi wa kaloleni waliojitokeza
kwenye mkutano wa kampeni za Uchaguzi jijini Arusha kata ya
kaloleni.Amesema wanakaloleni wasipoteze muda wao kwa kukipa nafasi
chama chochote cha upinzani.Amesisitiza atasaidiana na akiana mama wa
kata ya kaloleni keendeleza mifuko ya VICOBA ambayo ipo chini ya
serikali ya CCM |
 |
| Mh.Mbunge
Devotha Likokola akimnadi mgombea wa udiwani kata ya kaloleni Ndugu
Emmanuel Thomas kwa tiketi ya CCM.Amesisitiza hakuna mtanzania
asiyependa kufika ama kuishi Arusha,Lakini kwa huu upuuzi wa CHADEMA wa
kuvuruga jijini ni ishara tosha kwamba hawafai hatakupewa nchi.Hivyo
wanakaloleni wampe kura diwani wa CCM. |
 |
| Mh.Mwigulu
Nchemba,Naibu katibu Mkuu wa CCM amehutubia mamia ya wananchi wakata
ya kaloleni jijini Arusha jioni ya leo tar.8/6/2013 kwenye kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani.Mh.Mwigulu Nchemba ameanza kw akusema uchaguzi
unaofanyika sasa kata ya kaloleni ni matunda ya chama mufilisi cha
chadema kutotambua haki ya wananchi wanaopiga kura.Amesema CHADEMA
walifukuza diwani hapa,je kunahaja ya kuwapa diwani tena?AU
walipowafukuza walikuja kuomba ridhaa ya wananchi wa kaloleni?.Huu ubabe
kwenye vyama vya siasa ni wakupinga vikali na njia pekee ni kupiga kura
za kutosha kwa mgombea wa CCM. |
 |
| Naibu
katibu Mkuu wa CCM akisisitiza jambo kwa wananchi.Amesisitiza sana
kuhusu amani wakati wa uchaguzi na wakati wote wa maisha ya kila
siku.Amesema ni ajabu kwa Wana kaloleni na wanaarusha kukipigia kura
chama kinachoshabikia maauaji,CHADEMA wanashabikia mauaji,Chadema
wanatumia misiba kuhadaa wananchi na kutafuta sifa za kijinga.Pia
amewaomba wananchi kulaani vikali tabia ya Mbunge wa Arusha mjini
kutumia viroba kama fadhila kwa wananchi waliompigia kura.Amesema
thamani ya vijana wa Arusha sio viroba,Thamani ya vijana wa arusha ni
maendeleo na kudumisha amani. |
|
 |
| Hapa
Naibu katibu mkuua alikuwa anauliza,Je CHADEMA wamejenga angalau choo
cha jumuia hapa kaloleni?Pia akauliza ni kwanini CHADEMA hawafanyi
maandamano wilaya ya Hai na karatu?Akahoji zaidi kwa kusema je kunamzazi
anafurahia mtoto wake amwagiwe tindikali. |
 |
| Naibu katibu Mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea udiwani kata ya kaloleni kwa tiketi ya CCM Ndugu Emmanuel Thomas |
 |
| Hapa
naibu katibu Mkuu wa CCM akimpongeza mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM
kwa kuamua kujitolea kuwasaidia wanakaloleni na Wanaarusha kwa kupitia
CCM chama cha watanzania wote |
Mgombea udiwani kata ya kaloleni Ndugu
Emmanuel Thomas akiomba kura kwa wannachi na kuwaahidi kuendelea
kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo wanakata ya kaloleni na
jiji la Arusha
Post a Comment