Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua
gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za
taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya
Ruaha kandokando ya mto Ruaha wakipewa mafunzo hayo na wakufunzi
Martin Mthembu kutoka taasisi ya African Field Rager Training Services
ya Afrika kusini, kikosi hicho maalum cha TANAPA kilikuwa na askari 20
wamehitimu mafunzo hayo askari 19 moja hakufanikiwa kumaliza mafunzo
kwa sababu za kiafya, Kivutio kilikuwa kwa askari mwanamke pekee katika
kikosi hicho Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango
cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia ameza kufanya
mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa
alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu kutoka Afrika
Kusini na akampa sifa na pongezi nyingi kwa uwezo wake kama mwanamke. Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akirejea
meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo
hayo Kikosi hicho kikitembea kusonga mbele tayari kwa kutoa heshimza zao kwa mgeni rasmi. Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akipokea
heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya
kukabiliana na ujangili katika hifadhi za taifa kulia ni Adam Swai Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Iringa na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi
TANAPA Martin Loiboki. Askari
wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke
pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni
rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Frank
Anthon Malema kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na
kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe
Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na
kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi
akimpongeza John Kijazi baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo
hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.Martin
Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa
maelezo kwa Allan Kijazi Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa
TANAPA wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji
wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha
Nation Park. Askari
maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za
taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika
hifadhi hizo Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha Mkufunzi
wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho
katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu
Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi
wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher
Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park Mkufunzi
Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta
majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua
jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa
ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini
rudi salama Askari mwanamke pekee Aikande Lema akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangalia Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha. Mto ruaha Mnyama tembo yuko hatarini kutoweka kutokana na majangili kuwauwa kwa wingi wakichukua pembe zake
Twiga ni mojawapo ya wanyama ambao pia wanauliwa na majangili Mhifadhi
wa Ruaha Nation Park Paul Banga akitoa maelekezo kwa wahariri wa vyombo
vya habari kabla ya kuingia mbugani jana kwa lengo la kujifunza utalii
wa ndani na kujionea wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi
hiyo Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika geti la kuingilia kwenye mbuga ya Ruaha Nation Park.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUAHA NATION PARK
Post a Comment