Kampala, 02 June 2013
Mhe.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda
(Mb), asubuhi hii ameshiriki maombezi maalumu yaliyofanyika, Namgongo
nchini Uganda kwa ajili ya kumwombea Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere ili atangazwe mwenye heri na hatimaye Mtakatifu sawa na
imani ya dhehebu la Kikatoliki.
Maombezi
haya maalumu ambayo hufanyika kila mwaka, tarehe 1 Juni mwaka huu ukiwa
ni wa saba mfululizo, kuanzia mwaka 2007 katika kanisa hilo maarufu
nchini humo, ambalo limejengwa mahali ambapo Mfalme wa Baganda, Kabaka
Mwanga II aliamuru kuuwawa kwa Wakristo wapatao 35 kati ya miaka ya 1885
hadi 1887, walioifia imani yao na kukataa kumkana Mwokozi wao hata
mauti, alimaarufu Mashahidi wa Uganda, siku ambayo huandhimishwa kila
mwaka tarehe 3 Juni na kukusanya mahujaji wengi toka eneo lote la maziwa
makuu, wakiwemo mamia ya Watanzania.
Mgeni
Rasmi katika Ibada hiyo alikuwa Makamu wa Raisi wa Uganda, Mhe. Edward
Ssekandi, akimwakilisha Rais wa nchi hiyo, Mhe. Rais Yoweri Kaguta
Mseveni alisema licha ya sifa nyingi alizokuwa nazo Mwl. Kwa maisha yake
ya utuetezi wa haki za wanyonge na kupigania uhuru wa Mwafrika, pia kwa
uongozi wake mzuri uliompa sifa ndani na nje ya nchi yake, Wananchi wa
Uganda kamwe hawezi kumsahau kwa ajili ya vita vya Ukombozi wa nchi yao
vya mwaka 1978-79.
Pamoja
na Mhe. Spika, Kiongozi mwingine maarufu kutoka Tanzania aliyeshiriki
maombezi hayo na kuzungumza mbele ya Waumini hao wa Kikatoliki na
wengine wengi waliofurika kushuhudia tukio hilo alikua mwanasiasa
mkongwe nchini, Mzee John Samwel Malecela, ambaye aliwahi pia kuwa
Waziri Mkuu na Makamu Wa Pili wa Rais, chini ya uongozi wake, na kutoa
ushuhuda wa jinsi Mwalimu alivyokuwa Kiongozi mnyenyekevu na asiyependa
makuu, na hata kukataa kuitwa “Mtukufu Rais” kama ilivyozoeleka kwa
marais wengine.
Mama
Maria Nyerere na watoto wake Watatu, akiwamo mwanae ambaye ni Mbunge
wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, mbpia
walishiriki Ibada hiyo maalumu ambayo hutangulia Siku Maarufu ya
Maadhimisho ya Mashahidi wa Uganda inayofanyika Namgongo kila Mwaka.
Watu wengine maarufu kushiriki Ibada hiyo alikuwa Sika wa Bunge la
Afrika Mashariki, Mhe. Margaret Nantongo Zziwa, Wabunge wapatao sita
kutoka Bunge hilo la Jumuiya na wengine watatu kutoka Sudani ya Kusini.
Wageni
wengine maarufu waliokwishawahi kushiriki Ibada hii maalumu ya maombezi
kwa ajili ya Hayati Baba wa Taifa kutoka Tanzania ni pamoja na Mhe.
Benjamin William Mkapa, Rais Mtaafu wa awamu ya tatu, aliyeshiriki mwaka
2009 na Mh. Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg.
Jakaya Mrisho Kikwete aliyekwenda mwaka 2010.
Post a Comment