MKE wa naibu wa chifu
katika wilaya ya Marigat Alhamisi aliaga dunia katika hali isioeleweka baada ya
mumewe kumpata akinywa pombe haramu ya chang’aa katika nyumba ya
jirani.
Naibu wa chifu wa kata ya
Arabal Bw William Yegon inasemekana hakufurahia pale alipompata mkewe Bi Mary
Kobilo, 46, akipiga mtindi na wanakijiji wengine.
Wenyeji walioongea na
Taifa Leo walisema kuwa wawili hao walianza kuzozana wakati wa tukio hilo la saa
kumi na mbili jioni Jumatano huku naibu huyo wa chifu akimlaumu mkewe kwa
kumwaibisha kwa kunywa pombe hiyo haramu ilhali yeye alikuwa afisa wa serikali
anayefaa kuongoza vita dhidi ya pombe haramu.
“Naibu huyo wa chifu alikasirishwa sana kwamba mkewe alikuwa
akimkosea heshima licha ya serikali kutangaza vita kwa wapikaji wa pombe
haramu,”alisema mmoja wa wanakijiji ambao hakutaka kutajwa
jina.
Alisema kuwa baada ya
ugomvi huo marehemu alipepesuka nje ya nyumba lakini hakwenda nyumbani kwake.
Mwili wake ulipatikana katika msitu mmoja karibu na kwake Alhamisi
mchana.
Akithibitisha tukio
hilo,mkuu wa wilaya ya Marigat Bw Saul Moywaywa alisema kuwa uchunguzi tayari
umeanzishwa kubaini kiini cha kifo cha mwanamke huyo.
Sumu
“Mwili wake haukuwa na
alama yoyote. Tunashuku alijitoa uhai wake kwa kumeza sumu,”Bw Moywaywa
aliambia Taifa Leo kwa njia ya simu.
Mwili wa marehemu
ulichukuliwa na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya wilaya ya
Kabarnet kusubiri upasuaji
Post a Comment