Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Ban Soon-Taek wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe kwenye hoteli ya New Grand huko Yokohama nchini Japan tarehe 2.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe (kushoto) na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Moon Soon-Taek (katikati) wakati wa chakula cha mchana ambacho Mama Abe aliwaandalia wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa -Tokyo International Conference on African Development-TICAD V unaofanyika huko Yokohama nchini Japan tarehe 1-3.6.2013
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Mama Lordina Mahama, Mke wa Rais wa Ghana (kushoto) na Mama Ban Soon-Taek wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe kwenye hoteli ya New Grand huko Yokohama nchini Japan tarehe 2.6.2013.
Baada ya kupata chakula cha mchana wake wa Marais na wakuu wan chi za Africa wanaonekana wakibadilishana mawazo. Pichani ni Mama Lordina Mahama, Mama Salma Kikwete, Mama Moon Soon-Taek na Mama Sia Nyama Koroma, mke wa Rais wa Sierra Leone
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika wakiangalia maonyesho ya traditional calligraphy yaliyokuwa yakionyeshwa na wanafunzi mara baada ya chakula cha mchana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa high school baada ya wanafunzi hao kufanya maonyesho ya traditional calligraphy katika hoteli ya New Grand mjini Yokohama tarehe 2.6.2013.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiaagana na Mama Akie Abe, mke wa Waziri Mkuu wa Japan mara baada ya chakula cha mchana. Katikati ni Mke wa Rais wa Mali Mama Traore Mentou Doucouri.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Waziri Mkuu wa Japan Mama Akie Abe (wa kwanza kushoto) na wa pili ni mke wa Rais wa Namibia Mama Penekupifo Pohamba wakati wa chakula cha mchana huko Yokohama tarehe 2.6.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Post a Comment