Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher
Mtikila
---
Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda
kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha
akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea
binafsi.
Katika hukumu iliyosomwa jana jioni, mahakama
imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania
inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye
uongozi.
Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya
kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya
Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba
yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.
Post a Comment