WABUNGE wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Grace Kiwelu (Viti
Maalum) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa
Katibu wa CHADEMA Kata ya Sokoni One, marehemu Judith William Moshi, aliyeuwawa
kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni za chama hicho, Jumamosi iliyopita, Juni 15,
2013. Judith alizikwa jana kwenye makaburi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Sokoni one, mjini Arusha.
Wabunge wa Chadema wakiwa eneo la makaburi tayari kwa maziko ya marehemu Judith Moshi aliyefikwa na mauti baada ya kulipuliwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha Jumamosi hii.. Marehemu ameacha watoto watatu wa kike.
Kamanda mwenye tisheti nyekundu hapo ni Katibu wa Mbunge Godbless Lema, anaitwa Gabriel Kivuyo yuko ICU kwa siku ya tatu sasa hazungumzi kwasababu aliumia vibaya kichwani na miguu yote haina kazi! Tumuombee Mungu ampe uzima aendelee kulitumikia taifa.. Its so sad kwamba huyo mama aliyelala pembeni yake (akiwa marehemu tayari) baada ya mlipuko Kamanda Judith Moshi ndio amezikwa leo Sokoni 1, Arusha .. ni Kiongozi wa chama na kina mama na Katibu wa Chadema katika Kata hiyo. Judith ameacha mtoto wa miaka 2 na watoto wengine wa kike wote!
Post a Comment