15Wednesday, June 12, 2013

Polisi wa Kike aliyepiga picha za utupu atimuliwa kazi 
 
WP Amisa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imemfukuza kazi askari wake wa kike, WP Amisa, aliyekuwa akifanya kazi kituo cha Polisi Magomeni kutokana na utovu wa nidhamu.

 Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova amesema, Amisa amefukuzwa kazi kwa kuwa amekiuka maadili ya Jeshi kwa kitendo chake cha kupiga picha za utupu zilizoonekana katika mitandao.

Amesema, baada ya uchunguzi wa muda mrefu hasa baada ya taarifa na malalamiko ya watu kuhusu askari huyo, Juni 7 Jeshi hilo lilimtia hatiani askari huyo baada ya kujiridhisha na mwenendo mzima wa picha katika mitandao hiyo.

No comments:

Post a Comment