Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RIPOTI YA MGOGORO GESI MTWARA YAIVA.

 


Picture: Anbert Ngurumo na Charles Mwijage, DodomaPicha ya maktaba: Naibu Mhariri Mtendaji wa Free Media ambao ni wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari, Ansbert Ngurumo (kushoto), akibadilishana mawazo na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, Bungeni mjini Dodoma. (Picha na Erick Kabendera)

KAMATI Maalum ya kuchunguza mgogoro wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, imesema imefikia katika hatua nzuri baada ya kuwasikiliza watu wengi wanaohusika na mgogoro huo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Charles Mwijage ( Muleba Kaskazini-CCM), aliliambia NIPASHE mjini Dodoma kuwa kwa kiasi kikubwa kazi hiyo imekamilika.

“Tumeshaenda konana na watu wa site (Mtwara) na tumeshajua mambo mengi...timu yangu ilikwenda huko na kukus

anya taarifa, picha na sasa kilichobakia ni kwenda kuonana ana kwa ana,” alisema.
Alisema wamelazimika kurudi kwanza bungeni kutokana na umuhimu wa bajeti hiyo na akawatoa hofu Watanzania kuwa mahali walipofikia ni pazuri.

Kwa mara ya kwanza vurugu hizo zilijitokeza Januari 31 mwaka huu, kutokana mpango wa Serikali wa kujenga bomba kubwa la gesi kusaidia kupunguza tatizo kubwa la ukosefu wa umeme nchini.

Hata hivyo, hali hiyo ilitulia kwa muda na vurugu ziliibuka tena wakati Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospiter Muhongo, alipokuwa akisoma bajeti ya wizara yake hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Spika Anne Makinda, hadidu za rejea ni kuchunguza chimbuko la mgogoro, kufuatilia hatua zilizochukuliwa na Serikali kutatua mgogoro huo, kukutana na wadau mbalimbali ili kupata maoni yao kuhusu mradi ya gesi asilia na kuangalia mambo mengine yenye uhusiano na mgogoro huo.

Alisema kamati itapata nafasi ya kutosha ya kukutana na wananchi, vikundi, taasisi na watu binafsi.

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top