Mshindi wa
taji la Redd’s Miss Geita 2013, Salshia Isidore (katikati) akiwa mwenye furaha
wakati wa kupiga picha ya pamoja na warembo wqenzake Stella Magerezi (kulia)
aliyeshika nafasi ya pili na Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Nurieth Rashid.
Salshia aliwashinda warembo wenzake 12 waliokuwa wakiwania taji hilo pamoja
nae.
Warembo
waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya
pamoja.
Mbunge wa
Viti Maalum kutoka Mkoani Geita, Vicky Kamata (kulia) akitoa nasaha zake kwa
washindi na warembo wote walioshiriki shindano hilo.
Na
Father Kidevu Blog, Geita
MREMBO
Salshia Isidore amechaguliwa kuwa Redd’s Miss Geita 2013 baada ya kuwashinda
warembo wenzake 12 katika shindano lililifanyika Jumamosi Juni 1, kwenye
ukumbi wa Desire uliopo mjini Geita.
Wengine
walioingia nafasi ya tatu bora ni pamoja na Nurieth Rashid aliyeshika nafasi ya
tatu na Stella Magerezi alishika nafasi ya pili.
Katika
shindano hilo lililosindikizwa na burudani safi kutoka kwa msanii Baby Madaha na
Bob Haisa huku mgeni rasmi akiwa ni Mbunge wa Viti Maalum wa Geita Vicky
Kamata.
Washindi
hao watatu watawakilisha mkoa wa Geita kwenye shindano la Kanda ya Ziwa ili
kuwapata washiriki watakaoenda ngazi ya taifa.
Akizungumza
na washindi pamoja na warembo wengine kwa ujumla Vicky aliitaka jamii ya watu wa
Geita kuyatambua mashindano hayo kuwa ni muhimu na yanasaidia suala la
ajira.
Alisema
kuwa kupitia mashindano hayo kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika kwa kuwa
mashindano hayo ni fursa ya kuzungumza na wananchi kuielezea masuala mbalimbali
ya kimaisha.
“ Najua kwa
sasa hata katika Bunge hili la bajeti kuna mengi ambayo tumeyajadili na
kuyapitisha kwa ajili ya vijana na hasa pia kupitia sanaa na hivyo mashindano
kama haya yanahusika kabisa” alisema Vicky.
Naye
mwandaji wa shindano hilo alisema kuwa washindi hao mshindi wa kwanza amepewa
laki tatu, huku wa pili amepewa laki mbili na wa tatu laki tatu.
Post a Comment