Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TANZANIA YAPANDA VIWANGO VYA UBORA DUNIANI

 


TANZANIA imeendelea kutakata katika msimamo wa viwango vya ubora duniani ambavyo hutolewa na Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) baada ya kupanda kwa nafasi saba mpaka kufikia nafasi ya 109.

Kwa maana hiyo Tanzania sasa imekuwa ya pili kwa  nchi za Afrika Mashariki katika viwango hivyo huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Uganda ambayo ipo katika nafasi ya 93 baada ya kuporomoka kwa nafasi mbili mwezi huu.

Kwa upande wa tano bora za Afrika Ivory Coast wameendelea kuongoza kwa kushinda nafasi ya 13 duniani wakifuatiwa na Ghana ambao wako katika nafasi ya 22 na nafasi ya tatu inashikiliwa na Mali ambayo ipo katika nafasi ya 23. Wengine ni Algeria waliopo katika nafasi ya 35 kwa upande wa dunia huku tano bora kwa upande wa Afrika ikifungwa na Tunisia walioko katika nafasi ya 42.

Kwa upande wa orodha ya tano ya dunia ni Hispania ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina na Croatia wameendelea kubakia katika nafasi zao walizokuwepo mwezi uliopita wakati kwenye nafasi ya tano kuna ingizo jipya la Uholanzi ambao wamekwea kwa nafasi nne mwezi huu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top