Gari
la zimamoto likiwa eneo la tukio likizima moto ulioteketeza Ukumbi wa
Stereo leo mchana. Mashuhuda wa liokuwepo eneo hilo walisema kuwa Mtoto
huo ulioanza majira ya saa nane mchana umeelezwa kuwa umetokana na
hitirafu ya umeme iliyoanza baada ya kutokea cheche za moto wakati mmoja
wa wapambaji alipokuwa akiendele na kazi ya kupamba ukumbi huo kwa
ajili ya sherehe iliyokuwa ifanyike ukumbini hapo leo jioni.
Mashuhuda
wengine walitonya kuwa baada ya moto huo Mtungi wa gesi uliokuwa jikoni
pia uliripuka na kuongeza kasi ya moto huo. Aidha imeelezwa kuwa baada
ya moto huo, gari la zimamoto liliwasili eneo la tukio baada ya dakika
20 ulipotokea moto huo lakini, liliondoka bila kufanya kazi hiyo ya
kuzima moto baada ya kufika eneo hilo na kujikuta halina maji na hivyo
likaondoka kwenda kujaza maji na kurejea tena.
Hapa ni kwenye kona ya ukumbi huo kama inavyoonekana.
Mamia ya wananchi wakishuhudia moto huo ukiteketeza ukumbi huo.
Mmoja
kati ya waliojitokeza kusaidia kuzima moto huo akimwaga maji ndani ya
ukumbi huo kumalizia kuzima moto huo. Kwa picha zaidi bofya hapa chini
Majirani waliosaidia kuzima na kuhamisha vitu katika nyumba hii iliyo jirani na ukumbi huo.
Majirani
waliowahi kuhamisha vitu vyao vya ndani kabla ya moto huo kuanza
kusambaa katika nyumba nyingine, kwani moto huo umesambaa katika nyumba
tatu za jirani na eneo hilo, lakini uliwahi kuzimwa.
Majirani wakiwa nje ya nyumba zao....
Kijana wa Zimamoto akitandaza mpira wa maji ili kupitisha maji kuelekea kwenye moto huo.
Jinsi
moto huo ulivyoteketeza vifaa vyote ikiwa ni pamoja na viti vilivyokuwa
vikiandaliwa kwa ajili ya sherehe iliyokuwa ifanyike jioni ya leo
ukumbini hapo.
Baadhi ya vijana wakijisevia mabaki...
Na wale wa vyuma chakavu hawakuwa mbali, hapa wakikusanya mabaki ya vyuma....
Gari la zimamoto likiendelea kuzima moto huo.
Taswira ya ajali hiyo ya moto.
Sehemu ya wananchi wakiendelea kushangaa.
Bar maarufu Kinondoni iitwayo 'STEREO' imateketea kwa moto mkubwa sana
jioni ya leo. Moto huo unadhaniwa ulitokana hitilafu ya umeme katika bar
hiyo. Pamoja na bar hiyo kuteketea pia nyumba tatu lilizokuwa jirani
na bar hiyo pia zimeathirika na mali nyingi kuharibika.
Credits: Sufiani Mafoto & Jestina George Blogs























Post a Comment