CHANGAMOTO
zinazowakabili wajasiriamali wadogo katika utunzaji wa kumbukumbu na
kuwafanya wasiaminike, kupatiwa mikopo kwenye taasisi za fedha, ufumbuzi
wake sasa umepatikana.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mtaalaam wa
kutengeneza Mfumo wa Utunzaji wa kumbukumbu kwenye Kompyuta, Erick Muta,
alisema anashukuru kwa kupata tunzo hiyo ya dola za Kimarekani 328,000,
zilizotolewa na Mfuko wa Ubunifu (ICF).
Alisema
hivi sasa wajasiriamali hao wanaweza kutunza kumbumbu zao za mapato na
matumizi kila siku baadala ya kutumia madaftari kwa ajili ya kujua
alichoingiza na alichotumi.
Mutta
alisema mfumo huo (Min Shop), utawasaidia wafanyabiashara kwa
kuwajengea uwezo utakaowafanya wakidhi vigezo vya kibeki ambapo watawza
kukubalika katika kupatiwa mikopo kutokana na utunzaji bora wa
kumbukumbu zao.
“Hadi
sasa wapo baadhi ya wajasiriamali ambao wametumia mfumo huu ambao
umewasaidia katika kupata mikopo toka tasisi za fedha, vilevile
tunatarajia kuwatembelea watu mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia elimu
kuhusu mfumo huu jinsi unavyoweza kuwakwamua kiuchumi”alisema.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Sekta ya Ukuzaji Uchumi (FSDT), Sosthenes Kewe, alisema
mpango huo wa kuwajengea uwezo wabunifu na wajasiriamali ni endelevu
ambapo hiyo, ni mara ya pili kutoa zawadi.
Alisema
anaamini kuwa utasaidia katika kutanua wigo wa kupunguza ukosefu wa
ajira kwa vijana, ambao ndio kilio kinacholikabili taifa.
Mmoja
wa wafanyabiashara Zephania Mgonella, alisema, tangu alipoanza kutumia
mfumo huo ameweza kupata mafanikio katika utunzaji wa kumbukumbu zake,
hata anapotakiwa taarifa za kila siku na mwezi anazipata kirahisi ambako
hapo awali ilikuwa ni shida
Post a Comment